Ukiwa Likizo ukaugua huitaji Sicksheet kwakuwa siku unazotumia kujiuguza haziingiliani na muda wa mwajiri. Inapofikia Ugonjwa umepitiliza siku za Likizo na ukaingilia siku za mwajiri lazima umwagize mtu wa karibu akujazie Sicksheet na kukutumia ili uwe nayo huko huko unakotibiwa na kila unapohudhuria Hospitali uwe nayo Daktari aijaze kisawasawa kwenye Jedwali lake juu ya tatizo linalofanya uhudhurie Hospital, vinginevyo wewe ni mtoro na Unatakiwa uchukuliwe hatua za kinidhamu. Vilevile unapaswa uwe umetibiwa hospital ya Serikali ama sivyo pawepo na rufaa ya kwenda kwenye hiyo Private Hospital. Wajuvi ongezeeni.