Naomba kusaidia makadirio ya nyumba kwa ramani hii

Naomba kusaidia makadirio ya nyumba kwa ramani hii

virouzo

Member
Joined
Jun 23, 2021
Posts
16
Reaction score
6
Habari Wana jamii forum,

Nimeikuta sehem hii ramani nikaipenda nikaona si vibaya kushare mawazo nanyi kuhusu vitu vifuatavyo;
1. Idadi ya tofali kuanzia msingi mpaka boma
2. Idadi ya trip za mchanga kufyatulia tofali
3. Idadi ya sementi kujengea boma lote hadi lenta
4. Tripu za mchanga kujengea boma mpka lenta
5. Idadi ya mbao za kupaua
6. Idadi ya bati za kupaua
7. Idadi ya nondo za lenta na canop zote

Kama Kuna mapungufu pia yaweke.

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwenu

IMG_20210623_153323_949.jpg
View attachment 1828498View attachment 1828499
 
Nina nyumba kama hiyo tofauti ni kidogo sana

1.idadi ya tofali kuanzia msingi mpaka boma 2500 za inch 5 na 6
2.idadi ya trip za mchanga kufyatulia tofali 20 ila sikushauri ufyatue tofali, peleleza sehemu nzuri ukanunue
3.idadi ya sementi kujengea boma lote hadi lenta 60
4.tripu za mchanga kujengea boma mpka lenta 4
5.idadi ya mbao za kupaua 200 za ft 12 hapo ni 2x2 na 2x4
6.idadi ya bati za kupaua 60 zile za ALAF ndefu
7.idadi ya nondo za lenta na canop zote 45

haya makadirio yatategemea kina cha msingi wako na urefu wa kuta za nyumba yako kwenda juu

UKITAKA UFANIKIWE: anza kujenga na ulichonacho na usipige hesabu sana ukajikuta huanzi kwa kuhofia, anza na ulichonacho
 
Nina nyumba kama hiyo tofauti ni kidogo sana

1.idadi ya tofali kuanzia msingi mpaka boma 2500 za inch 5 na 6
2.idadi ya trip za mchanga kufyatulia tofali 20 ila sikushauri ufyatue tofali, peleleza sehemu nzuri ukanunue...
Shukrani kiongozi kwa mchango wako
 
Hivi nyumba ya vyumba viwili tu unawezaje kusema umeipenda?
 
Nina nyumba kama hiyo tofauti ni kidogo sana

1.idadi ya tofali kuanzia msingi mpaka boma 2500 za inch 5 na 6...

Jumla inacost shngapi?

Halafu apo kwenye kufyatua tofali, ni heri afyatue mwenyewe yanakua na resho nzuli ukilinganisha na yakununua.
 
Jumla inacost shngapi?

Halafu apo kwenye kufyatua tofali, ni heri afyatue mwenyewe yanakua na resho nzuli ukilinganisha na yakununua.
Jumla kwa haraka hapo aandae m20 ili ajenge na ahamie, nimejumlisha na madirisha, milango na shimo la choo kwenye hii hesabu yangu
 
siyo parefu kama utaamua kuanza na ulichonacho, mimi nilikuwa na milioni 3 nikaanza, nimepiga hesabu juzi nimegundua nimeshatumia milioni 30 na zaidi, ni suala la kuanza na ulichonacho tu mkuu, ukiangalia hesabu kubwa utashindwa kuanza
Shukrani kaka kwa kunipa moyo
 
Back
Top Bottom