Naomba kusaidiwa dondoo za uandishi wa nyimbo

Akaliza

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2022
Posts
227
Reaction score
239
Bila kupoteza muda naomba niingie kwenye mada tajwa. Ninatamani sana kujifunza uandishi wa nyimbo, licha ya kujaribu ku "Google" ili kupata muongozo nimejikuta sisogei mahali popote.

Kwa kuthamini uwepo wa Jukwaa la maarifa-JF, nimeona nije humu kuomba msaada wenu. Kama una tips za Uandishi wa nyimbo naomba uzishee ili niweze kujifunza.

Napenda zaidi aina ya uandishi wa wanamziki kama Billie Eilish, Khalid, Olivia Rodrigo na avicii

Natanguliza shukrani zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…