Naomba kusaidiwa kuhusu kodi ya kampuni

Naomba kusaidiwa kuhusu kodi ya kampuni

Mopalmo

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2010
Posts
534
Reaction score
139
Wana jf,kampuni yetu tulisajili tangu mwaka 2010,kutokana na hali mbaya ya biashara na mimi kuwa masomoni hatukuweza kulipa kodi kwa miaka hii yote na hatukutoa taarifa tukitegemea mambo yangekua safi badae,sasa angalau tumepata fedha kidogo,tunataka tulipe,swali ni je naweza kuepuka penalties,ili nilipe kodi ya awali pekee?

Maana zinazidi hata kodi yenyewe. nimeandika barua kuelezea sababu za kutolipa lakini bado sijaipeleka, nifanyeje wakuu,mawazo yenu yamekua msaada sana kwangu msichoke kunisaidia
 
mdau hata kama hamkuwa mnafanya biashara hamna budi kufanya marejesho ya kodi "Returns" kwanyinyi mlitakiwa muwe mnamarejesho sifuri yaani "Nill Returns" sasa kutotoa taarifa hizo hilo ni kosa lako lazima upigwe adhabu(penalty) la sivyo ungeweza kuwaandikia kabla kuwa hamkuwa mkifanya biashara yoyote na wao kujiridhisha.
 
Kwa hiyo unashauri nini mdau,ni jinsi gani tunaweza kupunguza tax burden
 
Mdau cha kukushauri ni kuonyesha nia ya kupunguza hilo deni lenu kwa mamlaka husika(TRA) kutoka hapo unaweza kumwandikia commissioner wa kodi juu ya suala lenu na baada ya wenyewe kujiridhisha wanaweza kuwafikiria juu ya hoja yenu.Mamlaka iko na haki ya kujua kama unafanya biashara au hufanyi kutoka kwa mfanya biashara mwenyewe yaani huo ni wajibu wako kuwajulisha juu ya biashara yako
 
Tafuta tax consultants wakushauri, acha ubahili.
 
Thanx kijereshi na wengine mlioshauri,nimeshaandika barua na jumatatu,nitaipeleka kwa commissioner,nitarudi hapa jf kwa mrejesho wa yatakayoendelea
 
Back
Top Bottom