Naomba kusaidiwa kuhusu upatikanaji wa mkopo kwa ajili ya kuanzisha biashara ndogo

Alex Hamis

Member
Joined
Jan 13, 2016
Posts
8
Reaction score
3
Hello! JF,

Kwa majina naitwa Alex Hamis, ni mwanafunzi wa chuo kidogo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha lakini kwa upande mwingine ni kijana ambaye napenda kujishughulisha na ujasiriamali, hivyo nimekuwa nikifuatilia fursa mbalimbali za kibiashara na kutokea kupata nyingi lakini tatizo/kikwazo kilichonikwamisha ni Mtaji lakini si suala la kunikatisha tamaa kutokupambana zaidi na zaidi, na ndipo nikapata wazo la kuwa na uhitaji wa Mkopo kutoka katika taasisi au kampuni yoyote ndani na nje ya Tanzania.

Hivyo nimeliwasilisha kwenu wadau mwenye kuweza kunisaidia katika hili anisaidie maana nina uhitaji mkubwa wa kuanza ujasiriamali huu ambao unanihitaji kiasi cha Tshs 960,000/=..

Nitashukuru sana kwa maoni au ushauri wako!
 
Tafuta saccoss, ni suluhisho zuri tu kwako... Wana VIGEZO nafuu kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…