Naomba kusaidiwa naona kama napata hasara

Benokolongokonongose

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
213
Reaction score
52
Hapa naomba ushauri.
Mimi ni mwanamke mjasiriamali. Shughuli yangu ni kununua ndoo za mafuta zilizoisha na kubadilishana na kuku wa kienyeji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji na Msumbiji kwenyewe hasa vijijini na mashambani.

Huwa natumia pikipiki san heroji. Sevis ya pikipiki na mafuta mara nyingi natumia sh 130000 hadi na 40 hivi. Kununua hizo ndoo huwa inanigharimu kama sh 50000 kwa mwezi. Ambapo wastani ni kama sh 190,000.

Nikishauza kuku huwa napata wastani wa sh 320,000. Ndani ya miezi hii miwili wa 5 na wa 6 biashara imekuwa ngumu kidogo naingiza wastani wa sh 270,000 hadi sh 287,000.

Naomba ushauri kwamba je niendelee tu au nitafute njia nyingine kabla sijaanza mwezi wa julahi?Mnaonaje wenzangu?
 
anza kuuza bangi ina faida sana
 
Wakuu Asprin na MO11 samahanini nilikosea kitufe cha kutuma nilibonyeza kwa bahati mbaya kabla sijamaliza maelezo. Kwa heshima nawasilisha.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…