Naomba kusaidiwa vitu vifuatavyo kuhusu hii biashara ya pikipiki

Naomba kusaidiwa vitu vifuatavyo kuhusu hii biashara ya pikipiki

mkimagii

Member
Joined
Oct 16, 2013
Posts
34
Reaction score
58
Wakuu, naomba kusaidiwa vitu vifuatavyo kuhusu hii biashara ya pikipiki.

1.Aina ya pikipiki uliyokuwa unatumia au aina ya pikipiki unayopendekeza kwenye hii biashara
2.Wastani wa pesa uliyokuwa unapata kwa siku au weekly.
3.Gharama yamatengenezo kwa siku au kwa mwezi

Natanguliza shukrani zangu kwawote wataojitolea kuchangia.

Asanteni.
 
Hii biashara haifai ilinishinda pamoja na kumiliki duka la spare Labda kama utaendesha mwenyewe
 
Hii ni biashara kichaa ambayo unakuwa stress siku zote, nimewahi kuifanya lakini nilijuta nikakonda nikaisha, kama wew mwenyewe ndio dereva piga kazi lakini kuwapa hawa wahuni achana nayo kabisa, bora ukalime.
 
1. Nunua TVS STAR HLX 125 ni bomba, ngumu kuharibika na zina ulaji mdogo zaidi wa mafuta (km 60 kwa lita 1).
2. Kiwango cha kuingiza inategemea na sehemu ya biashara yako.
3. Ukiwa mtunzaji gharama ya kuitengeneza ni elfu 8 (oil-6,000+fundi-2,000) kwa kila wiki au wiki 2.
(biashara ushindani usije lalamika ikiwa huna kipaji cha kuvuta wateja, ukishindwa saana nitafute kuna kampuni ipo special kukusaidia dereva, matunzo, kukulipa hesabu).
 
Mkuu bora ukafanya pikipiki ya mkataba. Yaani unaingia mkataba na dereva, unamnunulia pikipiki mpya, anakupa chako kila siku (vizuri akiwa unachukua kwa wiki), bima, service, ulinzi vyote juu yake. Akiingia kazini au asiingie wewe hesabu yako iko pale pale. Baada ya muda wa mkataba (mara nyingi kati ya miez 10 - 12) kuisha chombo inakua mali ya dereva
 
1. Nunua TVS STAR HLX 125 ni bomba, ngumu kuharibika na zina ulaji mdogo zaidi wa mafuta (km 60 kwa lita 1).
2. Kiwango cha kuingiza inategemea na sehemu ya biashara yako.
3. Ukiwa mtunzaji gharama ya kuitengeneza ni elfu 8 (oil-6,000+fundi-2,000) kwa kila wiki au wiki 2.
(biashara ushindani usije lalamika ikiwa huna kipaji cha kuvuta wateja, ukishindwa saana nitafute kuna kampuni ipo special kukusaidia dereva, matunzo, kukulipa hesabu).

You are very right Palantir...Naweza kukucheki kwa ushauri zaidi? asante
 
Back
Top Bottom