Naomba kuuliza, nataka kujua

Naomba kuuliza, nataka kujua

Mchuja Nafaka G

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Posts
763
Reaction score
253
Swali 1: Hivi Outsourcing Company, hupewa leseni kwa sheria ipi ya nchi?

Swali 2: Kwa nini kampuni hizi mfano ISON BPO hulipa mishahara kinyume na maagizo na maelekezo ya serikali?


Mfano, mwaka 2013, serikali kupitia katibu wa Wizara ya Kazi/Ajira, ilitoa agizo na maelekezo kwa ISON BPO, kuwa wao wapo ktk sekta ya mawasiliano kutokana na kazi ambazo wafanyakazi wake wanazifanya.
Kwa maneno mengine inatakiwa walipe mishahara ya kuanzia laki nne kwa wafanyakazi wake, lakini la ajabu kampuni hiyo imekuwa ikitunishia misuli serikali kwa kusisitiza kuwa wao hawapo ktk sekta ya mawasiliano, na imekuwa ikiwalipa wafanyakazi wake mishahara ya kati ya 150,000/- na 270,000/- kama gross salary kwa mwezi.
Je, hii ina maanisha nini?


Swali 3: Kipindi cha majaribio au probationary period ni miezi sita. Kwa namna ninavyoelewa, na baada ya kipindi hicho cha miezi sita, muajiri anatakiwa afanye tathmini ili kuona iwapo mfanyakazi huyo anafaa au la, kama anafaa, muajiri anatakiwa ampe mfanyakazi huyo mkataba wa kazi, na kama mfanyakazi huyo hafai, muajiri inatakiwa amuachishe kazi mfanyakazi.
Lakini ajabu hawa ISON BPO, wamekuwa wakiwatumikisha wafanyakazi wake kwa miaka miwili hadi mitatu bila mikataba, kwa hili sheria inasemaje?

Kwa wasioijua ISON BPO. Hii ni kampuni kutoka India, iliyoingia mkataba na Airtel Tanzania, ili kusimamia kitengo cha huduma kwa wateja kwa mambo ya data, airtelmoney na voice. Na kwa sasa wameingia kampuni ya mawasiliano ya TIGO na kampuni ya ndege ya fastjet kwa vitengo hivyo vya huduma kwa wateja.

*wafanyakazi wanaozungumziwa hapa ni wale wa huduma kwa wateja wa Airtel ila wapo chini ya ISON BPO*

Majibu kitaalamu tafadhalini.

NIMEONA SEHEMU HII HOJA NIMESHINDWA KUWA NA MAJIBU, NAOMBA MSAADA WENU WANAJAMII
 
Pole ila kua mpole tu, kama unapewa chochote kitu vumilia na endelea kuonesha bidii zaidi, utapewa mkataba tu, usije anza kuonesha jeuri kwa kuwa mkataba unachelewa utajuta. Hayo makampuni ndo hivyo tena, tumikia ------ upate mradi wako
 
Pole ila kua mpole tu, kama unapewa chochote kitu vumilia na endelea kuonesha bidii zaidi, utapewa mkataba tu, usije anza kuonesha jeuri kwa kuwa mkataba unachelewa utajuta. Hayo makampuni ndo hivyo tena, tumikia ------ upate mradi wako

Haki hutafutwa, haki haiombwi. Peleka swala lako kwenye shirikisho la vyama vya wafanyakazi.
 
Haki hutafutwa, haki haiombwi. Peleka swala lako kwenye shirikisho la vyama vya wafanyakazi.

Sawa pamoja na hayo, lakini kumbuka hadi hiyo kampuni inajiamini kulipa hivyo lazima wanajua kabisa zipo hoja na sababu ambazo hata akienda kushtaki, watazitoa huko na kueleweka, na ktk suala la kipindi cha kuangaliwa ni simple tu watasema hatujaridhika na utendaji wake, hivyo tumempa muda zaidi wa kumuangalia.

Ndo mana mimi nikashauri, awe mpole tu, ujeuri asioneshe, na kama ni kufuatilia afuatile chini chini kwanza asijeropoka na kuipoteza kazi, kumbuka wasomi ni wengi, atarudi kukaa kitaa na mwingine ashike nafasi. La msingi ni kuendelea kutafuta njia mbadala huku huko hapo unapata experience zaidi, wakati huo huo unafuatilia ili siku ukilipua bomu tu unakua na uhakika wa kupata haki yako.
 
Ila hyo kazi ya kupokea simu ni ngumu balaa. Kwa masaa nane unaongea na wateja 200 Mimi nilikuwa pale Ison BPO ya Tigo nilipoacha kazi masikio yakawa hayasikii vizuri. Naamini Mungu atawalipa kwa unyonyaji wao
 
Back
Top Bottom