Naomba kuuliza, ndugu zangu Waislamu na nyie mna maji ya upako?

Naomba kuuliza, ndugu zangu Waislamu na nyie mna maji ya upako?

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Kiufupi Imani zetu ni kali ila sipendi kutofautisha kwa kukejeli.

Leo nipo ofisini napitishiwa karatasi kuhusu huduma ya maji ambayo inaondoa mikosi.

Mtindo huu ulianza kwa wakristo kama kubatiza na mengine ila mbona unajirudia upande wa waislamu.

image-2022-05-27-1:20:38-830 PM.jpg
 
Ubunifu umeisha, now ni kuigana tu kilichobaki

Sadaka ni muhimu Ila siku hizi waumini hamtoi,so lazima mbinu km hizo zitumike ili mufungue mifuko
 
Huyo Ni mpuuzi mmoja mwenye njaa na mchawi aliyejifunza nyuma ya maji
 
Hakuna, inawezekana hao matapeli au waganga wa kienyeji kupitia mgongo wa dini.
 
Matapeli

ukifuatilia kwa karibu utakuta wana kadi za uanachama wa Bakwata
 
Hayo maji waliyosema masheikh wametaja yametoka wapi
Yale mengine ya pale Tanganyika Packers ni ya Canadian
Nadhani unaona tofauti
 
A/Alaykum ndg zng
Ujue mambo hayatofautiani sana maana asili ya hizi Iman zote ni hapo Mashariki ya kati/Middle East.
Ndio katika Uislam kuna maji ya zamzam na maji ya kisomo/dua.

Maji ya zamzam ni maji ya chemchem asili iliyopo mji mtakatifu wa Makka waislam wanaokwenda kuhiji mara nyingi huyabeba na kujanayo ila sio kibiashara na yanaminika kutibu na kuondoa matatizo mbalimbali.
Pia maji ya dua haya unachukua maji safi yaliyotwahara kisha ukayafanyia kisomo/dua na kisha kuyatumia kwajili ya tiba.
Wabillah tawfiq
 
Sulle nae ni mjanja janja fulani anaetumia mwamvuli wa dini, nimewasikiliza saana hawa, hata yule mazinge ni hivyo hivyo,ni wapigaji pesa kwa namna fulani hivi.
 
Dr. SULE ni mjanja japo namkubali kwa vitu vingine.

Jamaa ni mfanya biashara kama mfanyabiashara mwingine.
 
A/Alaykum ndg zng
Ujue mambo hayatofautiani sana maana asili ya hizi Iman zote ni hapo Mashariki ya kati/Middle East.
Ndio katika Uislam kuna maji ya zamzam na maji ya kisomo/dua.

Maji ya zamzam ni maji ya chemchem asili iliyopo mji mtakatifu wa Makka waislam wanaokwenda kuhiji mara nyingi huyabeba na kujanayo ila sio kibiashara na yanaminika kutibu na kuondoa matatizo mbalimbali.
Pia maji ya dua haya unachukua maji safi yaliyotwahara kisha ukayafanyia kisomo/dua na kisha kuyatumia kwajili ya tiba.
Wabillah tawfiq
Kwenye uislam hakuna mji mtakatifu,Bali Pana misikiti mitakatifu,ambayo ni miwili tu,wa Makkah na yerusalem...hii ni kwa mujibu wa quran
 
Walioko kwenye uislam ni wanadamu kama walioko kwenye ukristo halafu ujue shetani Hana dini yeye humtumia yeyote bila kujali dini yake ili kupotosha ulimwengu.
 
Back
Top Bottom