Naomba kuuliza vijana wenzangu kati ya kilimo na kubeti bora nini?

Erick MR

Member
Joined
Nov 11, 2022
Posts
77
Reaction score
159
Siku kadhaa zilizopita naibu waziri wa kilimo Anthony Mavunde katika mkutano na wahariri jijini Dodoma uliolenga kutekeleza ushiriki wa vijana katika kilimo cha biashara program itakayo ongeza ajira kwa vijana 3000 nakuongeza ukuaji wa sekta ya kilimo Hadi kufikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2030.

Nanukuu "Vijana wetu wanatamani kufanya kilimo lakini miundombinu yakuwafanya wakafanya kilimo haikua rafiki sana sisi tumeamua kukifanya kilimo kivutie na vijana watoke kwenye kubeti wakalime kwahiyo tulichoamua tuliweka mazingira rafiki kumfanya kijana avutike akalime tumeamua kusafisha maeneo nakuweka miundombinu .tutawasaidia miundombinu na kuwatafutia masoko " -Anthony Mavunde (Naibu waziri wa kilimo) .


 

Attachments

  • images%20(1).jpg
    9.5 KB · Views: 22
Yeye mavunde analima????Tuanzie hapo
Kiongozi hilo sina uhakika nalo na hatakama analima kilimo chake hakiwezi fanana na sisi vijana tunaotokea familia za hali ya chini lazima atakua amejitosheleza . Ila hawa tunaowaita viongozi wetu wanapaswa kujitafakari wanapotoa hizi kauli za kisiasa hawajui wanagusa hisia zetu kwa upande hasi.
 
Sasa kwa kifupi mdogo wetu mavunde ajipime kwa kauli zake asilete siasa kwenye maisha ya wadogo zetu wengine
 
Kubet si ajira.

ukilima unakuwa umefanya kazi ya uzalishaji mali..
Hapa nahitaji Somo kidogo kiongozi kubeti kunachangia Pato la taifa kwasababu ya Kodi naomba kufahamu Ili shughuli anayofanya mtu iitwe ajira au kazi inakuaje ?
 
Heri ulime uwe assured na food supply
Sijakataa kulima nachojaribu kung'amua hapa ni Naibu kurelate kilimo na kubeti. Kuna mifano kadhaa ya ndugu zangu ikiwemo mimi mfano nimeshatoa hapo juu. Na kuna ndugu yangu aliwekeza mara mbili kilimo cha ufuta na mpunga morogoro zaidi ya 3M na ushee kilichomkuta Hadi Leo hataki kusikia Siasa za kilimo .swali kwako je unahisi nchi yetu Ina mazingira shawishi na rafiki kwa kilimo?
 
Kubeti si kazi ni mchezo. Ili iwe kazi utakuwa unafanya analysis sana kitu ambacho kijana wa Tz sio rahisi awe na hizo resources.
Kweli ni mchezo ila unatumia analysis nadhani point yako ipo kwenye resources (rasilimali) hapo ndipo kwenye utofauti kwasababu kwenye kubeti Kuna makampuni hadi shilingi 1 mtu anabeti lakini kilimo unahitaji Mtaji ,Muda, Akili na Rasilimali watu kiufupi kilimo ni mchakato.
 
kilimo na kubet ni kitu kimoja
Hii point kubwa vyote ni sawa ila kimoja kinachukua Muda kuleta matokeo ya faida na hasara kingine kinachukua Muda mfupi. Mwalimu nyerere aliwahi kusema " Kupanga ni kuchagua" kwenye hotuba yake ya mkutano mkuu wa TANU Mei 28, 1969 na hili ndilo linalotakiwa Sasa watu waamue wenyewe. Sio Naibu waziri kuona kilimo ndo bora zaidi kuliko kubeti aache watu wachague.
 
huyo mzee sitakagi hata kumsikia shida za nchi hii mpaka leo yeye ndo chanzo
 
huyo mzee sitakagi hata kumsikia shida za nchi hii mpaka leo yeye ndo chanzo
Hili tuliweke kiporo tutalijadili siku nyingine kwa upana zaidi boss. sio wewe tu wengi huwa wanamaoni tofauti juu ya taifa letu haswa kwa uongozi wa hayati J.K Nyerere.
 
Kubeti sio kazi boss, hakuna kazi ambayo chanses za kutengeneza faida kulinganisha na mwenye kampuni kuchukua mtaji wako ni 90:10.

Kila unapokula unapata pesa yako + a certain % ya pesa yako. Kadri % inavyokuwa kubwa ndivyo ugumu wa kupata unavyoongezeka maradufu.

Ila ukipoteza unapoteza 100% ya ulichowekeza.
Hii unaiitaje biashara?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…