Naomba kuuliza vijana wenzangu kati ya kilimo na kubeti bora nini?

Bora kilimo
 
Leta hoja boss kusema bora kilimo haitoshi
Kilimo kinachangamoto yake lakini ukijipanga Lazima utatobo. Lima kwa malengo. Wekeza katika kilimo cha umwagiliaji. Tengeneza menejiment nzuri katika usimamizi mpaka mauzo. Betting sio kabisa. Katika betting Kuna nguvu Giza zenye nguvu sana ndio maana mikeka mingi huchanika kwa mechi moja tu, jiulize
 
Nionyeshe shamba la buku
 
Hapa duniani Kila kitu ni kubet tu,sema hizo betting zinatofautiana namna ya upotezaji hela au upatikanaji wa hela.
Betting zingine zinapoteza hela taratibu,zingine zinakupa hela taratibu.
Betting zingine zinakupa hela haraka na kupoteza hela haraka.
Ni uchanguzi wako,ni shughuli ipi ya betting unayofanya.
Kilimo ni kamari,kuwa mtumishi wa umma,au shirika binafsi ni kamari,kusoma ili baadae uje upate kazi ni kamari,kuoa au kuolewa eti ukiwa na familia utapata maisha mazuri hiyo ni kamari,
Kuzaa mtoto aje akusaidie baadae hiyo ni kamari,Kufungua biashara yoyote ni kamari.Kusafiri ni kamari,kupata kazi ni kamari.na kadhalika na kadhalika ..
Kwa hiyo unaweza kuona Kila kitu maishani tunachofanga binadamu ni kamari.
Ni swala tu la kuchagua ni kamari ipi ufanye.
 
Taifa la excuses litakuambia kubet ni bora kuliko kilimo wakija na justification za kitoto

Katika watu wote ninaowajua wote wanaobet nikiwauliza kati ya kula(profit) au kuliwa (loss)ipi imekutokea mara nyingi wengi husema wameliwa Sana so hakuna discussion kuwa betting ni upuuzi kama upuuzi mwingine

Kama umewahi kusoma probability kwenye hesabu huwez hata kujaribu kubet cause the system was made For you to loose
 
Aisee hakuna kilimo unachowekeza shilingi alfu tatu ukaondoka na zaidi ya milioni na nusu....kubeti ndio future yako kijana, jilipue mara moja moja

 
Oya eh msichukulie pw kilimo...june mwaka jana nmeuza kiroba(mpunga kg 90) 190k...

Halafu chaka nlitoka na vinjunga kama 195 hivi halafu nililima ekari 5 tu....na saiz nko chaka kama kawa
Mwaka Jana June? 2022?? Bei ya mpunga kwa gunia ilikua 190,000??? Kawaongopee watu wajinga tu

Hata mwaka huu tunalia bei ya mchele imepanda lakini gunia la mpunga halijafika 190000

Tanzania hii bei ya gunia la mpunga halijawahi kufika 190,000. Wacha kabisa huo uongo wako. Labda useme gunia la mchele
 
Heri ulime uwe assured na food supply
Hakuna assurance yoyote, kilimo chenyewe nacho ni kubet vile vile. Tena bora kwa mhindi unajua mkeka umeliwa siku hiyo hiyo au kesho yake kuliko kilimo unakuja kujua umeliwa after 3months.

Kilimo huna control ya supplies ya maji (mvua), na hata ukiwa nayo (kisima/mto) still bado ukishauvuna huna uhakika soko litakua limekaa vipi kipindi hicho na bado madalali wapigaji uwakwepe hapa ni zaidi ya kubet.

Bora tu usuke mkeka uweke timu zako mbili ukiliwa unajua poa umeliwa.
 
Bora kupata pesa
 
Biashara yoyote ni kubeti. Kilimo pia ni kubeti. Ila kubeti inatakiwa uwe na umakini katika kuchambua mechi, na kuchagua bet za kuweka. Na uwe na subira. Usiwe na papara za kuweka mkeka mmoja mreeefu mpaka miguuni ukitegemea kutia jero ule milioni 200.

Nenda hatua kwa hatua. Betia mtandaoni. Mechi moja tu kila siku. Hela usitoe. Baada ya mwezi utayaona matunda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…