Naomba kuunganishwa na mtu aliyeko China Kibiashara

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Wadau. Kuna bidhaa nimeiona alibaba lakini naona hapo dukani inauzwa kwa bei ya jumla.nami nataka kwa reja reja.

Nataka kumpata mtu wa uhakika aliyeko china mwenye ndugu hapa dar nimuagizie huko guangzhou ndiko duka kampuni husika ilipo.

Mwenye mtu wa uhakika naomba tuwasioiane inbox tujue tunafanyaje.maana najua matapeli wapo wengi sana kwa sasa
 
Itaje ni Ni bidhaa gani ili tujue kam anaweza kuinunua na kuja nayo...wapo wengi tu tena mwingine ameondoka jana baada ya week mbili atarudi.
 

Njoo pm nna ndg huko
 
Mtafute faiza all inta ndio Kaz anayofanya na kwa sasa yupo china.kwa maelezo zaidi ingia instagram.
 
wewe huwezi elewa maana hata kuandika kiswahili hujui . nenda kamwambie mtu mmoja akufundishe kuandika kiswahili. halafu uje hapa nikueleweshe. jinga kabisa . badala ya kuacha watu wenye akili wawasiliane na mimi unakuja hapa kutoa hewa chafu.


Huelewi unachokitaka utakua tapeli wewe.viatu viatu gani?vya kike vya kiume?pure leather product au vya aina gani? unataka kuulizwa maswali utazania mimi ndiyo mwenye shida..
 
wanapigwa vilaza. sisi wengine ni watu smart sana. zaid ya miaka 40 sijawahi tapeliwa nije nitapeliwe na washamba wa humu JF? wewe uwe unaangalia na watu kijana. kutapeliwa ni upumbavu wa mtu uliopitiliza.

dah, umejileta mwenyewe wacha upigwe
 
usihofu matapeli walikuwepo zamani siku hizi kuna vilaza tu. sikutapeliwa miaka ya 70s huko mpaka leo hii siwezi tapeliwa na hawa vilaza wa sasa. hawana akili ya kutapeli watu wenye akili.

Chizi kuwa makini usije ukapigwa.
 

Nami=namimi
Nimuagizie= nimuagize
Ilipo=ipo
Tuwasioiane=tuwasiliane

Mkuu kuhusu lugha tusichekane hakika nyani haoni kundule
 
nimuagizie unajua tofauti yake na nimuagize?
nami ni kifupi cha namimi. na inakubalika
ilipo ni sahihi soma sentensi nzima



Nami=namimi
Nimuagizie= nimuagize
Ilipo=ipo
Tuwasioiane=tuwasiliane

Mkuu kuhusu lugha tusichekane hakika nyani haoni kundule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…