Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,986
Kwenye jamii yoyote ile iliyostaarabika ni lazima kuwe na utaratibu wa kuwaongoza watu. Huu utaratibu ni muhimu ukakubalika na makundi yote katika jamii hii na hapa ndio katiba hutungwa. Wengi tumeona hata kwenye vikundi tu vya mtaani vya umoja wao huwa wanakuwa na katiba inayowaongoza.
Tanzania tuna katiba, lakini Katiba tuliyonayo ni ya zamani sana na ukweli ni kuwa kwa kiwango kikubwa haiendani na mahitaji ya sasa.
Nitatolea mifano ili nieleweke.
Katiba ilitungwa kipindi ambacho nchi yetu ilikuwa bado ina mfumo wa ujamaa. Na kwa sasa huu mfumo ni kama haupo. Katiba hii ilitungwa chini ya chama kimoja na hivi sasa tuna mfumo wa vyama vingi. Ni ukweli usiopingika kuwa kitendo cha raisi kuteua wafanyakazi wa tume ni cha ajabu sana, kwa kuwa siku ikatokea hata upinzani ukashinda kwa namna watayoijua wao basi ni wazi itawachukua nao miaka 60 kutoka madarakani Kama nyie CCM mlivyokaa.
Katiba ndio itakuwa suluhisho la kudumu kwenye kufikia haya yote, ni kwa nini raisi awe na mamlaka ya kuteua watu ambao wanapaswa kutoa haki hadi kwa watu ambao hawapo mlengo wa raisi?
Wateule wa raisi wanajikuta Wana kazi ya kumsifia na kumpamba raisi ili tu kulinda ajira zao. Raisi inabidi awe na mamlaka kidogo Sana ya kuteua au asiwe nayo kabisa na nafasi Kama za RC, DC, RAS, DAS, wakurugenzi, Makatibu wakuu hata mawaziri ziwe za kuombwa na ifanyike interview. Sio sasa ambapo kila raisi akija basi mteule ataji-switch na mfumo wa raisi mpya ili kulinda uteuzi aliopata matokeo yake tunajenda taifa la wanafki bila kupata Maendeleo yoyote.
Katiba mpya itatoa dira ya maendeleo kwa nchi hii. Nitawapa mifano.
Kipindi cha hayati mkapa alikuja na mfumo wa utawala wake akafanya yake akaondoka, akaja kikwete akafanya yake akaondoka, akaja hayati magufuli akafanya yake akaondoka na sasa yupo mama Samia nae anafanya yake.
Swali ni kweli tunahitaji twende kwa mwendo huu ambao kila raisi anakuja na kufanya yake anaondoka? Kila raisi anaingia na kuvunja ya utawala uliopita, kwa style hii nchi itapata maendeleo kweli?
Yote haya yanafanyika kwa kuwa katiba imempa mamlaka raisi ya kufanya anachojisikia.
Madhara yake ni kila raisi anakuja na vipaumbele vyake bila kujali wananchi wengi wanavitaka au laa.
Katiba mpya itajikita zaidi kuondoa mamlaka ya raisi kwenye kila Jambo badala yake wananchi ndio wataoanzisha mchakato wa miradi yote kupitia wawakilishi wao.
Mfano; wananchi wanataka ujenzi wa reli ya umeme, basi kutumia wawakilishi wao watapeleka hayo mapendekezo yao na mjadala utakuwepo bungeni na kuamuliwa. Tofauti na sasa hivi anayeamua miradi ni raisi.
Nimeona kuna watu wengi tu wa kutoka huko CCM wakilaumu Raisi kutaka kupitisha mradi wa bandari bagamoyo, sasa mjiulize kwa nini asipitishe ikiwa ana mamlaka hayo? Haya yote yasingewezekana ikiwa kuna katiba mpya ambayo ina-limit mamlaka ya raisi.
Na endapo atafanya tofauti na katiba inavyomtaka basi kupitia wawakilishi wenu ambao mmewachagua mnaweza kuwaambia wapige kura kutokuwa na Imani na raisi, kitendo ambacho kitafanya kiti cha uraisi kuheshimiwa.
Nyie watu wa UVCCM hebu tulieni na mfanye tathminj kwenye hili, katiba mpya haitakuwa sababu ya nyie kushindwa uchaguzi, kwani kama ni kweli watu wanawapenda na wanataka kuendelea na CCM watawachagua nyie, hofu ya nini? Ni wapi kwenye katiba mpya pataandikwa kuwa upinzani lazima ushinde? Acheni hii hofu tunataka kuona nchi ikisonga mbele.