Naomba kuwauliza, machache kwa hizi beti

Naomba kuwauliza, machache kwa hizi beti

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
Sheria
Niwaandikie tenzi, au naliwe shairi
Mpate na kulienzi, na mtoe ushauri
Mimi naitwa mkwezi, nasema nilofikiri

Naomba kuwauliza, machache kwa hizi beti
Na mpate kunijuza, haraka niende beti
Hawa wapo kutufunza, si kutupa tashtiti

Jamii yawaogopa, uhalifu haukomi
Kunao hao mapapa, wanaotupa vichomi
Wanatupiga mabapa, wajidai kwa uchumi

Wasimamia sharia, waivunjaje sharia
Akiumia maria, atalia saadia
Moyoni ninaumia, sina wa kunililia

Nakomea hapa hapa, nisije chana mkeka
Bado sinazo chapaa, ndo nafanya heka heka
Fikiri sitoke kapa, jibu muachie kaka


Abuuabdillah [emoji3578]
0744883353
Jumaomari5@gmail.com [emoji1241]
 
Hiyo sio beti acha kuigiza, ulisema una swali sa mbona hujauliza?
 
Karibu ndugu karibu, swali nimelisikia.
Natamani kukujibu, ila nashindwa ongea.
Ngoja nije taratibu, labda itasaidia.

Sheria na taratibu, zipo kutusimamia.
Toka enzi za mababu, ziliwekwa zikamea.
Leo ishakuwa tabu, sheria twazibomoa.

Hili jambo ni muhibu, amani linatishia.
Tena litatupa tabu, tukizidi kuchekea.
Muhimu kuliharibu, tuweze kuliondoa.

Utaona maajabu, ukikaa kuwazia.
Yule anaeharibu, ndiyo anaelijua.
Tena hukosa adabu, aibu humpotea.

Nisije nikaharibu, nikizidi kuongea.
Msiwene nina gubu, kwa mengi kuongelea.
Kwayo mi siweki jibu, mifano nishaitoa.
 
Karibu ndugu karibu, swali nimelisikia.
Natamani kukujibu, ila nashindwa ongea.
Ngoja nije taratibu, labda itasaidia.

Sheria na taratibu, zipo kutusimamia.
Toka enzi za mababu, ziliwekwa zikamea.
Leo ishakuwa tabu, sheria twazibomoa.

Hili jambo ni muhibu, amani linatishia.
Tena litatupa tabu, tukizidi kuchekea.
Muhimu kuliharibu, tuweze kuliondoa.

Utaona maajabu, ukikaa kuwazia.
Yule anaeharibu, ndiyo anaelijua.
Tena hukosa adabu, aibu humpotea.

Nisije nikaharibu, nikizidi kuongea.
Msiwene nina gubu, kwa mengi kuongelea.
Kwayo mi siweki jibu, mifano nishaitoa.
Anayelinda sheria ndio anayevunja
 
Back
Top Bottom