Poa, ukishajikagua uje ujibu swali la mtambuzi kwa ufasaha.
Kwa mfano inatokea mkeo au mpenzi wako anakuletea taarifa kwamba ameteuliwa na kampuni anayofanyia kazi akasome nje ya nchi, inaweza ikawa Marekani, Canada au kwingineko ambapo itamlazimu akae huko kwa miaka miwili mpaka amalize kozi yake. Lakini atakuwa anarudi likizo kila mwaka kwa mwezi mmoja.
Hebu niambieni kama inakutokea wewe unafanyaje?
Kiukweli itauma,maana unaweza kwenda kumpokea eapoti next likizo ukamwona ana mtoto wa kisomali!
hapa atakuwa bado mke wako au mke wenu?
Hapa kaka yangu Mtambuzi lazima itegemee!. Kuna mambo ya kuangaliwa hapa mfano watoto kama wapo itakuwaje? ataenda nao au watabaki na mimi na pia wana umri gani!. Kiujumla kwenye Ndoa hakuna anayependa kuwa mbali na mtu wake kwa umbali huo na kwa muda huo of course ndio maana ya kuoana, lakini yako mazingira ambamo lazima tuangalie 'opportunity costs' yaani ili upate hiki lazima ukose kile na hili upate kile lazima ukose hiki na hauwezi kuvipata vyote kwa pamoja.
Kwa sababu kila ndoa ni 'unique' na ni vigumu kusemea ndoa za watu wengine. Binafsi yangu kama nilivyosema hapo juu 'nitamruhusu' lakini prior to the mazingira yatakavyoruhusu!
wanagonga na mimba yake, kwani inang'ata?? mi wakati nna mimba yangu, kuna mshkaji ofisini na kulia alikuwa analia kwamba ye ugonjwa wake ni pregnant women, yaani yupo radhi kufanya chochote!! we dunia hii watu wamedata usisikie kabisa!Piga mimba kabisa aende nayo huko.Kitu muhimu sana hii mkuu
Mkuu nakubaliana na maoni yako, lakini hebu tufanye ni mchumba na mko kwenye michakato ya kufunga ndoa au ndio mmefunga ndoa mwaka mmoja uliopita (Na Ndoa bado haijajibu) halafu anapata hiyo nafasi ya kwenda ughaibuni kuongeza ilmu, na wewe ni mwajiriwa ukiwa na nafasi ya kawaida tu...........Hii ina maana kwamba akirudi cheo kitapanda na responsibility zitaongezeka lakini pia atakuzidi kipato.......... Hebu niambie hapo unachukua uamuzi gani?
lakini hebu tufanye ni mchumba na mko kwenye maana kwamba akirudi cheo kitapanda na responsibility zitaongezeka lakini pia atakuzidi kipato.......... Hebu niambie hapo unachukua uamuzi gani?
Nafatana nae.