Naomba maelezo juu ya hawa wanaokiita MKIKITA isije kuwa wao ni kama Namaingo

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
1,982
Reaction score
2,931
Kuna hawa wanajiita MKIKITA naona nao wana project kama za Namaingo we unatoa fees wanakuchukulia mkopo wanakulimia wanakata gharama za ulimaji na mkopo we eti unapewa faida tu.
Nikitazama naona kama ni Namaingo katika another form naomba mwenye ushuhuda anisaidie
 
"we unatoa fees wanakuchukulia mkopo wanakulimia wanakata gharama za ulimaji na mkopo we eti unapewa faida"
kitu kama hiki hakiwezekani kwani risk itakuwa mkikita.... hamna organisation ya kibongo inaweza kufanya hili.
katafute maelezo yao ya kina nina uhakika wa 95%+ risk itakuwa kwa mkulima.
 
Hata mimi hainiingii akilini aisee sema kuna mtu hapa ameshatoa ela basi najaribu kumwelewesha kuwa ni kama namaingo maana eti nao wanaambiwa wanataftiwa mikopo sijui wamesaini mikataba sawa na namaingo tu
 
Kuna hawa wanajiita MKIKITA naona nao wana project kama za Namaingo we unatoa fees wanakuchukulia mkopo wanakulimia wanakata gharama za ulimaji na mkopo we eti unapewa faida tu.
Nikitazama naona kama ni Namaingo katika another form naomba mwenye ushuhuda anisaidie
Wanakukulimia wewe ukiwa mjini unakula AC? Hakuna kilimo cha aina hiyo Duniani. Hizo ni triki za kupiga wale wavivu wote.

Kama unawekeza kwenye Kilimo wekeza wewe kama wewe.

NAMAINGO walipiga sana pesa make walikuwa nao wana hubili asali.
 
Hata mimi hainiingii akilini aisee sema kuna mtu hapa ameshatoa ela basi najaribu kumwelewesha kuwa ni kama namaingo maana eti nao wanaambiwa wanataftiwa mikopo sijui wamesaini mikataba sawa na namaingo tu
wanapiga sana pesa za watu wasio weza kuwaza
 
Yani huyu mtu wangu wa nne anapigwa wengine walipigwa na namaingo kwenye kilimo na ufugaji wa sungura huyu naye anapigwa kwenye kilimo na hawa yani too good to be true
 
Taarifa zaidi nenda ofisini kwao watatujuza kwa undani then unafanya maamuzi.
mbegu ya muhogo wanauza 200,000/= ya kutosha ekari moja (kwa wakulima ~ 80,000/=) unaweza kuambiwa uifuate mkuranga na wewe upo kibaha!
 
Hiyo inakula kwa mkulima Kuna jamaa yangu alilima mihogo alilipa gharama ya milioni 1 na nusu kapata hasara hajapata kitu na hao mkikità wameona story hivyo imekula kwake. Ucjalibu Lima mwenywwe
 
Kuna hawa wanajiita MKIKITA naona nao wana project kama za Namaingo we unatoa fees wanakuchukulia mkopo wanakulimia wanakata gharama za ulimaji na mkopo we eti unapewa faida tu.
Nikitazama naona kama ni Namaingo katika another form naomba mwenye ushuhuda anisaidie
*TANGAZO KWA WALIOWEKEZA KWENYE MIRADI YA BLOCK FARMS - MKIKITA.*

TAREHE YA *MWISHO* YA KUPOKEA BARUA ZA KUOMBA KUREJESHEWA FEDHA NI KAMA IFUATAVYO:

1. MUHOGO *Tar 30/04/2018*
2. MCHAICHAI *Tar 30/04/2018*
3. KIBITI B/Farm *Tar 10/05/2018*
4. FUKAYOSE B/ *Farm Tar 10/05/2018*

Ni kwamba kama wanarudisha pesa, kama hivyo basi sio matapeli
 
Back
Top Bottom