Sheria za Tz ni pasua kichwa sana mkuu, zimekaa kimagumashi makusudi ili kuwaneemesha wanasheriaNa hii inakiuka Ibara ya 13 ibara ndogo ya 6 kifungu c ya katiba ya jamuhuri ya muungano.Mtuhumiwa hana hatia hadi pale atakapotiwa hatiani na mahakama kwanini kumshikilia? Ikithibitika mahakamani kwamba hana hatia nani atafidia kuzuiliwa kwake?
Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini mkuu,sheria yoyote ikikiuka katiba ni batili kama ilivyokuwa katika kesi ya Peter Ngomango dhidi ya AK Mkangwa na Mwanasheria mkuu wa serikali,pale ambapo kifungu namba 6 cha sheria za mwenendo wa shughuli za serikali(GPA) 1967 kuwa ni batili kwa kukinzana na Ibara ya 30 ya katiba ya muungano.Kwenye kesi ya Dominic Mnyaroje aka Mbushuu dhidi ya Jamuhuri,hukumu ya kifo kwa mujibu wa kifungu 197 cha sheria ya makosa ya jinai pamoja na kukinzana na ibara ya 14 ya katiba bado ilikubaliwa kuwa hukumu sahihi.Hapo ndo penye utata.Ukienda ibara 64(5) ya katiba ,inasema sheria zote lazima ziitii katiba na sheria yoyote kinyume na katiba ni batili.Lugha gongana.Sheria za Tz ni pasua kichwa sana mkuu, zimekaa kimagumashi makusudi ili kuwaneemesha wanasheria
Mkuu,unageuza JF kuwa mahakama na kuharibu uzi wa watu kwa maswali na majibu. Kimsingi,kesi za madai hazipitii polisi. Lakini,waweza kuwapa notisi unaotaka kuwashtaki.
Mkuu,umeyasoma maoni yangu kwenye nambari 29? Yapitie kwanza halafu useme ulivyosema au ubadili.Wakili msomi petro mbona huku kwenye fani yako hupendi kujibu hoja za wanajamii? Uku uko vizuri tunakutegemea, lakini umekimbilia kulianzisha la akina mbowe huku ndo kwako fafanua hayo
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwakuwa nakuheshimu sana, nayapokea majibu yako.We nae dume zima unakua na nyooodo!!
Mtu kauliza swali, kama hutaki kujibu kaa kimya, kama hujui majibu sema sijui.