Naomba maoni: Binti wa Kichaga Kutoroshwa!

Naomba maoni: Binti wa Kichaga Kutoroshwa!

Kongosho

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2011
Posts
35,991
Reaction score
24,211
Kwanza samahani kwa kutumia jina la kabila kwenye kichwa cha habari, nimeweka ili kupata maoni barabara sababu mitazamo ya kutorosha binti ili kumuoa inaweza kuwa inatofautiana kati ya kabila na kabila.
Kwa wasukuma ni kitu kinachotokea mara kwa mara kwa hiyo si tatizo sana.

Mr Masanja (30's) kampa ujauzito Manka (20) ambaye anaishi na baba mdogo(Mr. Masawe). Kinachonishangaza huyu binti hataki Masanja aende kwao kujitambulisha anang'ang'ania atoroshwe tu.

Swali langu likabaki, je hii mila ya kutorosha binti ipo kwenye mila za kichaga? Kama ipo ndio njia rahisi kusuluhisha 'case' kama hii?

Nawaza kwa nini binti asimweleze mama yake ili liwe wazi na Masanja akajitambulishe na kumuoa?

Please, msaada!
 
wanaishi wapi?
mila kama mnaishi Sinza au magomeni ni tofauti
na kuishi Kishumundu
 
huyo msichana bado mdogo,asimsikilize atafute watu wazima wakaonane na wazazi wa huyo binti....
 
Eeh, huyo Binti vipi, anakataa mtu anayetaka kwenda kujitambulisha kwao, simwelewi kabisa, anataka timbwilitimbwili la kumtafuta mjini!
Kwanza samahani kwa kutumia jina la kabila kwenye kichwa cha habari, nimeweka ili kupata maoni barabara sababu mitazamo ya kutorosha binti ili kumuoa inaweza kuwa inatofautiana kati ya kabila na kabila.
Kwa wasukuma ni kitu kinachotokea mara kwa mara kwa hiyo si tatizo sana.

Mr Masanja (30's) kampa ujauzito Manka (20) ambaye anaishi na baba mdogo(Mr. Masawe). Kinachonishangaza huyu binti hataki Masanja aende kwao kujitambulisha anang'ang'ania atoroshwe tu.

Swali langu likabaki, je hii mila ya kutorosha binti ipo kwenye mila za kichaga? Kama ipo ndio njia rahisi kusuluhisha 'case' kama hii?

Nawaza kwa nini binti asimweleze mama yake ili liwe wazi na Masanja akajitambulishe na kumuoa?

Please, msaada!
 
Labda nyumbani wanamfahamu meku na yeye kashakubalika kwa mama kumuowa manka tatizo sasa manka ampend meku ,moyo wa manka upo kwa masanja.jf kutaja wachaga ni kawaid asubuh kuna kabila nimeltaja moderator wakaniwekea ** baadae wakaifuta comment kabisa
 
Hii strategy bado inafanya kazi? nadhani dingi na maza walitumia hii strategy ngoja Babu aspirin aje kutoa yaliyomo
 
Mie ni Mchagga, but simuelewi mwenzangu, ana tatizo gani hasa, kutoroshwa!, naona anajishushia heshima yake kama binadamu, atoroshwe kama Mbuzi!, kwanini asihamie mwenyewe kwa Masanja kama vipi!
 
wote wanaishi hapa Dar.
Tatizo mahusiano yatakayojitokeza.

Masanja anaishi kwa kaka yake karibu na baba wa Manka, ni majirani kabisa.
Mie nimewaambia watakosanishwa majirani na binti wa miaka 20 bila sababu.

Wafuate procedure.

wanaishi wapi?
mila kama mnaishi Sinza au magomeni ni tofauti
na kuishi Kishumundu
 
Mwanaume anapomtorosha Mpenzi wake kwao analeta ugomvi na anajishushia heshima kwa wakwe zake na jamii kwa ujumla, anaonekana ni tapeli na muhuni, hajielewi kabisa, hana heshima na hajastaarabika hata kidogo
 
hainiingii akilini atoweke home labda kwa wiki, aanze kutafutwa, tensiona kwa familia yake, sijui wakatoe taarifa polisi.

Mie sijawahi ona binti wa aina hii au hataki olewa.

Mie ni Mchagga, but simuelewi mwenzangu, ana tatizo gani hasa, kutoroshwa!, naona anajishushia heshima yake kama binadamu, atoroshwe kama Mbuzi!, kwanini asihamie mwenyewe kwa Masanja kama vipi!
 
Yeah, wafuate procedure, wasiwasumbue na kuwatibua watu, na kujishushia heshima wenyewe kwa kutokuwa wastaarabu
wote wanaishi hapa Dar.
Tatizo mahusiano yatakayojitokeza.

Masanja anaishi kwa kaka yake karibu na baba wa Manka, ni majirani kabisa.
Mie nimewaambia watakosanishwa majirani na binti wa miaka 20 bila sababu.

Wafuate procedure.
 
Huyo Mwanaume aact as a grown up man, asimsikilize kila kitu huyo binti anachomweleza, pengine bado utoto unamsumbua zaidi, awe mstaarabu kwa wakwe zake, asijishushie heshima
 
Back
Top Bottom