Kwa uzoefu wangu Vitz inasifa hizo unazosema, kwanza ni gari inayotumia mafuta vizur pia chini imekaza sana hata kama njia ni mbovu haiharibiki ovyo kama swift, pia kama ninkwa safar ndefu nunua vitz yenye injini ya 2nz zipo nyingi tu ina cc 1290. Swift pia ni nzuri ila haitaki kabisa njia mbovu aiseee,
huko chini inaharibika mno ukipita njia mbovu halaf na spare zake bei imechangamka japo zipo, kuna ndugu yangu alinunua showroom swift alikuwa anakaa kivule kma n mwenyej wa dar bila shaka utakuwa unapafaham,
ebana kila mwezi alikuwa ana kazi ya kuabadili spare huko chini baada ya muda tu kidogo mara shock up zimekufa, mm nilinunua gar mkononi tu kwa mtu namba C ila yy alinunu showroom ila alibadilisha spare za kutosha ndani ya muda mfup wakati mm nikawa na dunda tu, swift na rough road ni mwiko kabisa.
Starlet ni nzur pia sana ila tu ina injini ya kitambo ishapitwa na wakati, pia ulajia wake wa mafuta huwezi linganisha na vitz au swift, kwa sasa hv nunua gar yenye vvt-i injin zipo poa sana kwenye matumizi ya mafuta, pia hata shape ya vitz ni nzur kuliko starlet. Huo ndo uzoefu wangu mkuu. Uamuzi ni wako boss