Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Nimefurahi sana kuona Mheshimiwa Dkt Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa Fedha akijitokeza hapa jukwaani kuja kutoa ufafanuzi wa hoja ambayo ilikuwa inagusa wizara yake.Nampongeza sana kwa ujasiri na uthubutu wa hatua hiyo. kwa kuwa hatua hiyo inasaidia kuondoa uzushi , Uongo,taharuki na sintofahamu kwa wananchi.
Ikumbukwe ya kuwa uongo ukiachwa uzungumzwe sana pasipo kujibiwa unaweza kuaminiwa na baadhi ya watu hususani wasio jishughulisha kutafuta ukweli na wakaanza kuamini kuwa ndio ukweli wenyewe.
Ningependa Mawaziri wengine pia Waige Mfano huu uliofanywa na Mheshimiwa waziri .lakini pia napenda kumpongeza sana na kumtia moyo Mheshimiwa Dkt Dorothy Gwajima ambaye yeye sote tunafahamu ya kuwa amekuwa akija bila kusita kutoa ufafanuzi humu jukwaani hususani jukwaa la habari na hoja mchanganyiko.
Tena ingependeza Zaidi wizara zikawa na akaunti zao humu rasmi kwa ajili ya kuelezea masuala mbalimbali yanayokuwa yanatokea au kufanywa katika wizara zao.Lakini siyo tu kuwepo bali kuwa hai wakati wote.
Kikubwa na Rai yangu kwenu waheshimiwa Mawaziri ni kuwa tu na ngozi ngumu kwelikweli muwapo humu jukwaani, maana kuna watu wa kila aina humu jukwaani na wenye lugha za kila aina ambazo zingine unaweza kuhisi kukereka. wavumilieni wote na wala msiwajibu kwa namna watakavyo wajibuni au kuwashambulia.
Maana unaweza ukaandika jambo zuri au ufafanuzi wa jambo zuri halafu ukashangaa mtu anakurukia na kukwambia pasipo ushahidi kuwa wewe ni fisadi,jizi ,mla rushwa na huna akili.kwa hiyo usipo kuwa na kifua na ngozi ngumu utajikuta unapandwa na hasira na jazba na kuzira kabisa kuingia humu jukwaani.Maana wengine unakuta amejaa msongo wa mawazo au ana chuki tu binafsi na wewe au anakuchukia tu bila sababu hata ufanye lipi zuri atakuchukia tu.
Mfano mimi unakuta bila kosa mtu ananitukana matusi ya nguoni kabisa.Lakini huwezi kunikuta nikipaniki au kujibu kwa jazba au kuzira au kuchukia au kurudisha matusi au kumshambulia mtu zaidi ya kujibu kwa busara mfano namwambia mtu kwa upole tu kuwa nimekusame,Mungu Akubariki,asante kwa mtizamo wako,Uwe na Maisha marefu,pole kwa nilipokukwaza,tuvumiliane na kukosoana kwa staha na majibu mengine ya aina hiyo.
Kama waziri unajuwa una presha au hasira au jazba au kukosa subira , uvumilivu na kifua .basi nakushauri usiiingie humu jukwaani kwa jina lako maana utajikuta umejibu watu hovyo na kujipalia mkaa au kujishushia heshima yako na kudharaulika sana.kwa hiyo kama wewe huna kifua na Moyo kama wangu basi ni bora usomage kimya kimya tu na kupita kimya kimya.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.