naomba mawazo yenu jf.

naomba mawazo yenu jf.

isiaka

Member
Joined
Jun 1, 2012
Posts
17
Reaction score
2
ndugu zangu nataraji kupata jiko au mke wa kuoa sijui wenzangu ambao mpo katika ndoa naomba ushauri wa mambo gani nizingatie kwa huyo mke ili niweze mfaidi sio kujitui tena hyo ndoa.?
 
Jitoe mazima kwa mkeo.
Uwe mtendaji zaidi kuliko mtegemea kutendewa.
Wanawake wanathamini vitu vidogo2 ambavyo unatumia muda mwingi kuvifanya kuliko mavitu Makubwa ambayo unayafanya bila kumfikiria au ikifikiri atayafurahia just because umetumia pesa nyingi.

Mwisho ni kuaminiana!
 
Kama umeshafikia hatua hiyo hakikisha kuwa tayari umeshakubali majukumu yote kama ambavyo baba yako mzazi alivyokuwa akifanya ilakubwa kuliko yote ni kumtanguliza mungu pasipo kusahau uaminifu,mapendo na kuheshimiana,mengine yote yatafuata
 
asante kwa wale wenye mawazo positive na hao wengine poa kwa majibu yenu
 
Kaka usijisahau kujituma kama comandoo, ukijakuta mabazazi mengine huko nje yakakusaidia yatakuletea demeji. Wadada wa siku hizi si kihivo, si kama mama zetu, walikuwa wakipenda wamependa, akiolewa kaolewa. sikuhizi utasikia mafiga matatu na mapepo yake. Kuna kicheni paty moja nillichungulia juzijuzi nikagundua si kicheni paty ila ni kicheni mapepo. Imenitoa hata ile stimu ya kuoa.
 
Hongera Kaka, ukishashauriwa, washawishi na wenzio watuoe na sisi wengine jamani!
 
Back
Top Bottom