Naomba mawazo yenu!

Kashaija

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2008
Posts
255
Reaction score
62
Nina swali linanitatiza, hivi mke wangu ni ndugu yangu au rafiki yangu?

Tafadhali nisaidie.
 
Nina swali linanitatiza, hivi mke wangu ni ndugu yangu au rafiki yangu?

Tafadhali nisaidie.

Ukishajua na kupata jibu itakusaidia nini Kashaija? Nadhani swali lako halina jibu sahihi, ni uamuzi wako tu kama utamchukulia mkeo kuwa kama ndugu au rafiki. Pima kati ya hayo mawili na uamua utamchukuliaje.
 
She is both your friend & your relative. Kama ndoa yenu ipo kama inavyo paswa kuwa basi ni rafiki yako kwa sababu atakua wa kwanza kumuambia kila kitu chako na pia ni ndugu yako kwa sababu ndugu kufaana si kufanana. Nani wa kwanza kuku saidia kama si mkeo? Iwapo ndoa yenu ipo kama inavyo stahili kuwa atakuwa ndugu na rafiki yako. Lakini hali haipo hivi kwa wanandoa wote kwa bahati mbaya.
 
Inategemea uhusiano na ukaribu wenu ukoje..mwengine anaweza akawa zaidi ya ndugu, zaidi ya rafiki au vyote. Wakti kwa mwingine anaweza asikaribie hata kimojawapo..angalia uhusiano na ukaribu wenu ulivyo, utapata jibu.
 
Nina swali linanitatiza, hivi mke wangu ni ndugu yangu au rafiki yangu?
Tafadhali nisaidie.

Mke ni ndugu na pia ni rafiki.
Nilisikia/kuambiwa kuwa mke ni mpangaji (Kama mpangaji wa nyumba). Sikukubaliana na hii tafsiri maana kuna ndoa zingine mume anaweza kuwa mpangaji!
 
both.....

Mimi nadhani mwanamke ni rafiki na wala siyo ndugu. Nasema hivi kwasababu ndugu hana substitute, so long as amezaliwa akiwa ndugu yako ni ndugu yako tu! hukupanga wewe awe ndugu yako ila ilitokea wazazi wako ndo wakamzaa hata yeye. Hata akifa pengo haliwezi kuzibwa na mwingine atakayezaliwa.

Kwa upande wa mke, kuna substitute, ikitokea mungu akamuita kabla yangu naweza baadae kuoa mke mwingine na tukapendana kama au hata kuzidi yule wa kwanza. Hata yeye nadhani ananiweka kwenye kundi hilo la urafiki, maana nikitangulia mimi najua pia yeye anaweza kuolewa na bwana mwingine wakapendana zaidi ya mimi na yeye.
 
Nina swali linanitatiza, hivi mke wangu ni ndugu yangu au rafiki yangu?

Tafadhali nisaidie.


inategemea umemuoa nani! kama umeoa mtoto wa shangazi yako ni lazima awe nduguyo. laa sivyo mkeo ataendelea kuwa rafiki yako maishani.
 

Nimekusikia ndugu yangu ila bado nasisitiza kuwa ni both rafiki na ndugu kwa misingi ifuatavyo:
1. Hakuna uhusiano complicated ku define kama huu wa mke na mume kama ni ndugu au rafiki.Kwangu mimi ni ngumu kuweka cut off point kuwa huyu ni ndugu tu au rafiki tu.
2. Rafiki wa opposite sex atakuwa na mipaka - hivi ndugu yangu inawezekana vipi huyu rafiki aje akuangalie hadi sehemu nyeti pale say utakapohitaji msaada mathalani kwenye ugonjwa?
3. Ndugu yako pia wa opposite sex - mfano mama yako mzazi au dada yako hawezi kulala na wewe kitanda kimoja au hata kukupa huduma zile zenye kutaka faragha.Nimeshuhudia mama mmoja akimuuguza baba yake mzazi.Kwa vile mumewe hakuwepo, yule mama ilibidi kuomba msaada wa jirani wa kiume kumwogesha baba yule kwa vile mama yule aliona ni kukosa staha kuona utupu wa mzazi wake.
4. Mkeo mnapochanganya damu kwa kuzaa watoto basi undugu hukolea zaidi maana tayari watoto wana damu zenu na vinasaba.
5.Ukizaa na dada yako utakuwa gumzo katika jamii na pia sheria itakutia hatiani.
Kwa msingi wa haya machache ndiyo nikasema mke ni ndugu na rafiki at the same time mradi kila kitu kinabakia sawa.Kifo kikiingia basi kila mmoja wenu anakuwa huru lakini hata pamoja na hayo bado kutakuwa na link ya undugu kama mna watoto.
 
Nina swali linanitatiza, hivi mke wangu ni ndugu yangu au rafiki yangu?

Tafadhali nisaidie.

...mkishaoana na kuwa mwili mmoja ndio mshaunga undugu huo, lilobakia jitahidi umfanye mkeo Rafiki yako, ...utafaidi!
 
Nina swali linanitatiza, hivi mke wangu ni ndugu yangu au rafiki yangu?

Tafadhali nisaidie.

Kiimani/Kidini Mkeo ndiyo wewe maana maneno matakatifu ya Bibilia yanasema nao hawatakuwa wawili tena bali mwili mmoja.

Kimaisha ya kawaida inategemeana mahusiano yenu ndiyo yataweza kuwafanya muonekane kama mke na mme tu, mke +mme+ rafiki, mtu na mwenzi wake.

Mke na mme: mahusiano yanapokuwa yanatawaliwa na itifaki za ndoa zaidi kiasi kwamba hakuna mitoko ya pamoja ila kwa matukio maalumu tu, hakuna kutaniana, nk.

Mke + mme + rafiki: Mahusiano ya itifaki za kindoa yanakuwepo lakini siyo yale ya kihafidhina kwa maana kwamba wawili wanaweza kufanyiana matani lakini pia wawili hawa hushirikiana katika kupanga mipango yao mbalimbali kwa pamoja na kwamba kuambatana pamoja kwao ni kitu cha kawaida, n.k.

Mtu na Mwenza wake: Hapa wawili hawa hata kutambulishana mbele za watu kuwa ni mke na mme inakuwa ngumu wakati mwingine.
 

Inawezekana rafiki wa jinsia tofauti akaweza kukusaidia hadi kwenye sehemu nyeti lakini siyo ndugu yako. Na hili ndilo linalomfanya mke asiwe katika kundi la ndugu. Lakini pale inapokuwa hakunabudi huwezi kumwacha kumsaidia nduguyo wa njinsia tofauti halafu akafa eti kwa kuogopa kuangalia nyeti zake. Chukulia wewe ni Daktari pekee wa Kituo cha Afya halafu kaka yako akawa amepatwa na tatizo kwenye nyeti zake ambapo inahitajika afanyiwe upasuaji wa haraka vinginevyo atakufa, WoS utamwacha kakaako afe eti kwa kuogopa kushika tango/bamia lango/yake?
 

ukimfanya ndugu hutakuwa humlali tena
 
he swali la ajabu!!
mke ni mke, mume ni mume tu, kwani lazima awe kimojawapo?
mke/mume si ndugu wala rafiki.
Si ndugu, kwani han\mjazaliwa katika ukoo mmoja
Si rafiki, kwani mmeapizana mbele ya mungu na ndugu, kuanza uhusiano tofauti,

au unaweza wewe kuuliza hivi mjomba ni shangazi? au ni mama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…