Naomba mbinu za kupata maduka mengi ya rejareja ya vipodozi kwa ajili ya kuwauzi vipodozi kwa bei za jumla

EP MEDICS COSMETICS STORE

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2015
Posts
2,826
Reaction score
4,593
Wataalamu wa biashara ya vipodozi, ninaomba kusaidiwa mbinu mbalimbali za kupata maduka ya vipodozi vya aina zote yanayo-uza rejareja na mbinu za kuwafanya wawe wateja wangu kwa ajili ya kuwafanyia delivering ya vipodozi wanavyokuwa wanahitaji. Pia locations ambazo ninaweza kupata maduka mengi ya vipodozi ya rejareja

Natangiliza shukrani

Nilipo DSM
 
Ndiyo eneo nalozeekea hili

Ni biashara nzuri hii ukijua kanuni

1. Jiepushe na vipodozi kemikali hasa TBS walozuia

2. Jua aina za ngozi na changamoto zake ili uwashauri wateja kiuhalisia

3.mtaji kuanzia milioni 3 hadi 5 kukupa faida ya milioni kwa mwezi ni kawaida

Kwa ushauri bure piga 0713 039 875
 
Acha utani upate faida ya milion kweli?
 
Kwanza point of correction kusema unataka kusambaza vipodozi aina zote siyo kweli

Labda Kama ni dalali na siyo mmiliki wa duka la jumla au importer.

Nipo kwenye cosmetics ili uweze kusambaza vipodozi kwa bei nafuu inabidi uwe unaingiza mzigo mwenyewe, uweze kushindana na soko.
Lakini pia unatakiwa uwe specific kwenye aina ya vipodozi unavyotaka kusambaza.

So far vipodozi kutoka
Congo/zambia
South Africa
Nigeria
Uk
USA

Ndo vinavyouzika zaidi, je unaweza kuimport aina zote kutoka kwenye hizo nchi?
Kama unaweza Karibu sokoni.
 
Huwa naitaman sana hii biashara,hiv kwa 10m unaweza kufanya kweli?
 
Shukrani sana. Nitakucheki mkuu
 
Naagiza mwenyewe vingi ni toka india na dubai kwasasa.
 
Huwa una michango mizuri sana linapokuja swala la biashara ya vipodozi, Mungu akubariki.
 
Mchawi ni kutake risk mfano mimi mwaka 2010 nlikuwa naagiza apple toka south canter nzma then nasambaza kwenye maduka na supermaket morogoro kwa mkopo baada ya week naanza kukusanya mpunga wangu.

Nilijikuta nawauzia apple mpka viduka vidogo sabab mtu alikuwa hawez kaa na product ya apple week nzma bila kuuza so sjajua kwenye vpodoz ikoje na nkaja kujua kuwa wabongo wengi wanapenda mikopo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…