Nina mdogo wangu wa kiume ambaye amemaliza kidato cha nne 2011. Hata hiivyo, nahisi kama hakutendewa haki kutokana na shule ambayo amepangiwa kwa masomo ya kidato cha tano na sita. Pamoja na kufanya vizuri mtihani wa kidato cha nne kwa kupata Division I Point 16, huku akiwa na Physics C, Chemistry A, Mathematics A na Biology C; bado kwa masomo ya kidato cha tano amechaguliwa kwenda shule ya kata (Changombe Day) kwenda kusoma PCB!! Dogo, ambae hata miaka 18 hajafika (anatimiza August) amekuwa very disappointed hasa akizingatia wenzake ambao ama wamefanya vizuri sawa nay eye na hata waliofanya vibaya kuliko yeye wakiwa wamechaguliwa shule mzuri (angalau kwa majina)!! Mbaya zaidi, kwa zaidi ya miezi miwili sasa, tayari ameshapiga tution za Advanced Mathematics na Physics kwavile alitarajia kwenda PCM Boarding School! Leo hii anaambiwa aende PCB. Binafsi, sina matatizo na PCB na tangu zamani nilikuwa namshawishi sana asome PCB lakini alikuwa anakataa katakata na kutamka bayana kwamba ana mahaba ya dhati na Maths!
Kwa jinsi ilivyo nafahamu itatuwea ngumu kumwamisha toka Changombe kwenda Boarding School au shule yoyote iliyo nafuu kuliko Changombe ambayo kwa matokeo ya mwaka jana (A-Level), hawakuwa na One hata moja, bali TWO chache. Division III, IV na Zero ndizo zilitapakaa pamoja na shule hiyo kuwapo kilipo Chuo Kikuu cha Ualimu!!! Mbaya zaidi, hakuna pesa ya kumpeleka Private School. Hivyo basi, ushauri ninaoomba kwa wadau, je nini nafuu kati ya kumwacha hapo hapo Changombe au kumpeleka DIT ( Dar Tech)?! Binafsi, nilikuwa nafikiria kufanya mpango wa kumtoa Advanced School (Changombe) na badala yake aende Dar Tech ili akamilishe ndoto zake za kusoma ama Computer au Telecommunication.
NAWAKILISHA!