Naomba mlejesho kwa watu walio wahi kuagiza vitu kupitia usafirisha wa DHL

uzio usio onekana

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2019
Posts
836
Reaction score
2,658
kuna simu nataka kununua aliexpress na wasafarishaji wake ni DHL na inaonekana hawa jamaa sifa yao kubwa wako faster sana. wananiambia ndani siku 15 ninakuwa nimeisha ipata simu yangu. na simu yenyewe ambayo nataka kununua inauzwa sh million 1 na ghalama ya usafirishaji ni sh 89000
Lakini kwa upande wa pili nikajaribu kusoma post za miaka miwili nyuma kwa watu waliowahi kuagiza vitu DHL kuna mdau mmoja anasema aliagiza laptop dollar 250 kwa kupitia DHL na ilipo fika tena wakamkwangua sh. 190000 sasa akilini nikasema inamaana huyu jamaa hiyo laptop alinunua mara mbili. na inasemekana wapo watu ambao wamewahi kuvizila vitu vyao hukohuko DHL baada ya kuona gharama za usafilishaji ni kubwa mno. na nasikia wao wanafanya kazi kwa ukaribu mno na TRA
Lakini nikaona sio mbaya ni shee na waTanzania wenzangu ambao mmewahi kuagiza vitu kupitia DHL na inwezekana labda kwasasa wamejirekebisha
 
na inasemekana wapo watu ambao wamewahi kuvizila vitu vyao hukohuko DHL baada ya kuona gharama za usafilishaji ni kubwa mno. na nasikia wao wanafanya kazi kwa ukaribu mno na TRA
Nimewahi telekeza mzigo baada ya tozo kufikia TZS 550,000
Wakati thamani ya mzigo ( manunuzi na kusafirisha) ilikuwa ni chini ya TZS 350,000 : Angalia hapa: https://www.jamiiforums.com/threads...njia-ya-mtandao-online-purchase.743134/page-2
gharama za usafilishaji ni kubwa mno.
Hii gharama ukishalipa wakati wa manunuzi hakuna gharama nyingine ya usafirishaji.
na nasikia wao wanafanya kazi kwa ukaribu mno na TRA
Hakiki, iwapo bidhaa uliyoagiza inatakiwa ulipie kodi/ vat - hakuna jinsi inabidi ulipie.
na inwezekana labda kwasasa wamejirekebisha
Tatizo sio DHL, (hata ungetumia kampuni nyingie) tatizo lipo kwenye tozo za kodi/vat - wao DHL watasimamia na kufautilia clearance ya mzigo , hizo gharama utakazo lipia.

Kumbuka mzigo iwapo inatakiwa kulipia kodi/ vat - Ni jukumu lako kulipia, tena kwa wakati ili upate mzigo wako
 
Nashukuru kwa majibu mazuri
 
Kuvizila=kuvizira

Usafilishaji=Usafirishaji

by the way agiza tu huo mzigo wako maana inaonekana una pesa nyingi.I am sorry in advance.
 
Nilitaka kuagiza saa za kuuza...nikaenda Dhl wakaniambia nitakatwa VAT 18% na Importduty 25% ya thamani ya mzigo.
 
Ninawashauri unapoenda kulipia hizo tozo za tra DHL please hakikisha umechukua assessment document halisi za TRA acknowledgement of payment document from TRA.
Zinagatia sana ushauri huu. Mimi ni shuhuda wa hili jambo. Niliagiza mzigo wa laki 650,000 nikachajiwa kodi 390,000 na DHL. Nikawalipa.
After there nikawaomba wanipe document za TRA wakaanza kunizungusha na kuniambia ninachopewa ni risiti tu ya DHL. Nilikataa nikacommand nahitaji nipate hizo document. At the end wakaona wanipe. Kuangalia receipt za tra na assessment nikakuta kodi niliyochajiwa ni 108,000 tu.
Niliwadai hiyo ziada na kuandika barua kwenda kwao nikawapa muda iliwasiporespond niwapeleke sehemu wanayostahili. Thanks be to God walinirudishia.

Kingine cha muhimu usilipe hela kwa Cash, lipa kwa mpesa through their Mpesa number. Wafanyakazi wao wengi sio waaminifu, pia Mpesa itakusadia kupata reference ya malipo uliyolipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…