1.Shirika la benki la taifa.
2. Shirika la taifa la benki
Mie nadhani kwa ufahamu wangu sentesi hizi mbili zinabeba maana mbili tofauti,
unaposema Shirika la Benki ya Taifa hapa unataka kuonyesha kwamba, shirika hili ni la Benki yaani unataka kutoa utambulisho kwamba, hili shirika ni la benki na linahusiana na masuala ya benki na . Sentesni ya pili ya Shirika la taifa la benki, hii ni fasili na maana ya kwamba, shirika hili ni la taifa kwa maana kwamba, hili ni shirika la taifa yaani sio la binafsi na kadhalika, kwa hiyo unatoa utambulisho juu ya shirika la taifa ambalo linahusiana na masuala ya Benki.