hiyo robo huwa inafidiwa kwa kuweka mwaka wenye siku 366 ambapo hutokea mara moja kila baada ya miaka minne na hiyo tarehe si nyingine bali ni tarehe 29 ya mwezi wa february ambayo hujitokeza mara moja kila baada ya miaka 4 kufidia hilo pengo.
Kinachofanyika ni makadirio; Dunia inakamilisha mzunguko wa kulizunguka jua kila baada ya siku 365 na robo. Ikaonekana kuwa italeta usumbufu kuhesabu hiyo robo. Ikaamuliwa hizo robo siku zikusanywe ili kufanya siku moja nzima, hivyo kusababisha kuwepo kwa mwaka mfupi wenye siku 365 na mwaka mrefu wenye siku 366 unaotokea kwa kila miaka minne.
sawa nimekupata utata upo hapa mwaka mkubwa mwezi wa pili unakuwa na siku 29 na mdogo unakuwa na siku 28 tunaona kuna tofauti ya siku moja na siyo robo sasa naomba unifahamishe hiyo robo inafidiwa vipi mpaka mwaka mdogo uwe na robo ndani yake,maana robo ni masaa 6 sasa yamepatikana vipi.
Kwa kawaida kuna mwaka mkubwa na mdogo,ikiwa mkubwa una siku 366 na mdogo una siku 365 na robo.Ikiwa mwaka mpya unaanza tar 1/1 kila mwaka saa 6:00 usiku na unaisha saa 5:59 usiku tar 31/12 kila mwaka.Utata upo hapa kwenye mwaka mdogo ambao una siku 365 na robo. Je,ni kwa nini kuna robo na wakati siku ina masaa 24 na nikipiga mahesabu kwa mimi sioni robo.Je hiyo robo imepatikana vipi jamani wasomi,naombeni majibu nisaidike jamani.