Naomba mnisaidie kwa wanaofahamu hii kitu je ina ukweli?

karv

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2019
Posts
1,802
Reaction score
3,253
JINSI YA KUTAMBUA TAREHE AMBAYO MJAMZITO ANAWEZA KUJIFUNGUA

Habari za wakati huu

~Ukianza na tarehe yako ya mwisho ya hedhi toa miezi 3 halafu jumlisha siku 7

Kwa mfano:kama tarehe ya mwisho ya hedhi ilikuwa tarehe 10 mei ukitoa miezi 3 itakuwa februari 10 na ukijumlisha siku 7 itakuwa Februari 17 hivyo uwezekano wa mama kujifungua itakuwa tarehe 17 Februari

Maana kama kuna mtu anataka anichezee mchezo hivi

 
What if mwili utatumia mechanism zake kujiamulia kutenda??
 
SUBIRI TAREHE YAKO IFIKE USHUSHE MZIGO, ACHA KUBET... MENGINE MUACHIE MUNGU
 
Ingia google andika Pregnancy Due date calculator utaandika tarehe ya mwisho ya hedhi na watakuletea due date na baby gender

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 

Ni hesabu za kawaida zinazotumika kukadiria uwezekano wa tarehe ya mjamzito kujifungua. Lakini, kwa wale wenye uhakika wa tarehe ya alipoanza hedhi ya mwisho.
Njia ni mbili ya mwisho ni nyongeza:
1: Tarehe ya mwisho kuanza hedhi na mwezi husika.
(Jumlisha siku 7 na miezi 9).

2: Tarehe ya mwisho alipoanza hedhi.
(Jumlisha siku 7 na utoe miezi 3).

3: Tumia kipimo cha ultrasound ndani ya miezi mitatu ya mwanzo.

NB: Majibu yote +_2weeks. Using'ang'ane iwe siku hiyohiyo, ni makadirio.
 
Ni makadirio, wiki ya 40. Ila anywhere kuanzia wiki ya 36/37 ni normal.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…