Matumizi yote ni sahihi, lakin ni vizuri zaidi kutumia kama ifuatavyo:
1. Ikiwa nomino inayotajwa ni katika kundi la I-ZI kama vile, njia, barabara, kanzu, nazi, gari n.k. ni bora kutumia NDIYO. Mifano: Njia hii ndiyo uliyoichagua mwenyewe. Gari ile ndiyo iliyopata ajali
2. Ikiwa nomino inayotajwa ni katika kundi la A-WA na U-I, kama vile kijana, mfanyakazi, akinamama, mti n.k, ni bora kutumia NDIO. Mifano: Vijana uliotaka waje ndio waliofika. Mti uliokata ndio hasa niliokutuma. Akinamama ndio walioitwa hapa, wewe dume umekuja kufanya nini?
3. Kama unaandika neno moja tu, basi ni vizuri kuandika NDIO badala ya NDIYO. Mfano: Swali- Utakwenda Arusha kesho? Jawabu- Ndio.
4. Wakati tunapotamka, tukataka tusitake, tunatumia NDIYO kwa sababu itakuwa vichekesho kusema NDI-O.