Naomba mnitafsirie maana ya haya maandishi ya Kingereza

Naomba mnitafsirie maana ya haya maandishi ya Kingereza

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
Nielezeeni kwa kina hapa haya maandishi yanamaanisha nini

FB_IMG_1718696858631.jpg
 
MAAJABU YA KWELI
NI ni kwa jinsi gani Amri Kuu za Mungu kwa Moses mwaka 1300 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu,zilikutwa kwenye kitabu cha Misri kiitwacho " kitabu cha wafu" kuanzia miaka 700 iliyopita
 
Maajabu Halisi
Jinsi Amri za Mungu alizompa Musa miaka 1300 Kabla ya Yesu kupatikana Huko Misri" katika kitabu cha Mizimu" katika miaka ya 700 ya awali
 
Hayo ni mambo ya yule jamaa aliyekua mkalimani kwenye msiba wa JPM.
Majina kuwekwa kwenye makabati yote ya Africa
 
AFRIKA ndipo Miujiza yote ya Dunia ilipofanyika. Ikiwemu unga'amuzi wa maadili ya Binadamu.[✓] Pamoja na Ukaribu wa Mungu.
==============≠======

Unafikiri UBUNTU umetoka wapi?

Ubuntu ndio Ten Commandments.

Maarifa na Elimu yametokea Afrika na Ushahidi wake unapatikana na Homo Sapiens na sio Neanderthrals(ushahidi upo neanderthrals walitokomea kwa kukosa maarifa).

Na ieleweke, kuanzia Sayansi ya Anga, mpaka Hisabati, Ukemia, Utabibu n.k ulianzia Afrika, mpaka pale wazungu wakiongozwa na Mrumi kwanza alipochoma Alexzandria Library Egypt na baadae wazungu wengine kubomoa Timbuktu Library- zote zikiwa na hazina kubwa ya Elimu za kale(Esoteric) na ambazo zinaendelea kutumika leo hii. Including the Ten Commandments.

Kama Mwafrika Natembea kifua mbele.
 
Hapa kwa tafsiri sisisi utafeli. Isipokuwa the concept behind ni kwamba, Moze alipewa amri 10 miaka 1300 kabla Yesu hajazaliwa. Cha ajabu amri hizo hizo kumi ziliwahi kuandikwa kwenye kitabu kingine miaka 700 kabla Moze hajapewa hizo amri. Ndio kusema the book of dead kiligundulika kuwa na amri hizo miaka 2000 kabla Yesu hajazaliwa.

Swali ni je, Kama Moze hakuwa wa kwanza kupewa hizo amri 10, wa kwanza alikuwa nani, na alipewa na nani?
 
Muujiza wa kweli
Ni vile amri kumi za Mungu alizopewa musa miaka ya 1300,zilikutwa huko Egypt kwenye kitabu cha wafu,mapema mnamo miaka ya 700.

nimejipinda sana kutafsiri hapa sasa namimi nifanyie muujiza wa soda...😂
Umejitahidi sana japo umesahau kuandika BCE baada ya 1300
 
Ya nini tuhangaike na maandishi yaliotungwa na mjinga mmoja huko hata hatujui ni nani na chanzo chake ni nini!!!
 
Back
Top Bottom