ni vigumu kutoa ushauri hapa, kwasababu anayeongea siye aliyedhalilishwa, bali mtoto wa aliyedhalilishwa. angeliongea mama yako hapa, tungesema vingine, lakini unaongea wewe tena kuhusu mama yako. kwani kama ni kweli mama yako aliteleza kwa kosa hilo, unafikiri angekuja kukuaga wewe kama anaenda, au angekueleza wewe mtoto wake kwamba anafanya jambo kama hilo, jambo hilo huwa linafanyika kwa siri na si hadharani ikizingatia tena mme wa mtu...nashauri usilipuke sana kumtetea mama yako, wakati mwingine huwa inawezekana hao watu wakawa na ushahidi mzuri tu, either wa meseji walizoandikiana, au wa picha kukutwa laivu, na mambo mengine mengi tu ambayo wanaweza wakawa hawajayatoa hadharani. wanapata wapi ujasiri wa kusambaza habari hizo hadi kuwaambia watoto wake? tuseme kweli hawana akili timamu hata wakachukua uamzi mzito kama huo? lazima kuna sababu tu, kaeni chini mjichunguze kabla ya kuchukua hatua. what if ninyi mkienda kufungua kesi ya defamation ili mama yako alipwe kwa kudhalilishwa na kuchafuliwa reputation? halafu wao wakaja na ushahidi mzurii ulionyooka kuonyesha kuwa kitu hicho kilikuwa cha kweli? si itakuwa aibu mara mbili? nashauri mama yako ajichunguze, akae chini ajichunguze kabisaaa, ajiulize kwanini asingiziwe yeye tu tena na mume wa mtu jambo ambalo si la kawaida, baada ya hapo, kama kweli, mbele za Mungu atakuwa na uhakika kuwa kadhalilishwa bila sababu yeyote, afanye haya hapa chini.
kudhalilishwa kwa kuchafuliwa jina mbele za watu ni tort ya defamation, anaweza kufungua kesi ya madai mahakamani. lakini ajabu yake, dafamation ina defence mojawapo kuwa, kama kitu kilichosemwa ni cha ukweli, basi hawezi kuja kushinda hiyo kesi, ndio maan anasema isije kuwa wanao ushahidi wameuhifadhi, wameanza tu kubip ili mtu akipiga wao wamwage kabisa ugali na mboga, kama ni kitu cha kweli mtaumbuka. kama mama yako anahisi ni kweli kuna jambo hilo, potezeeni, endeleeni na maisha wala msipoteze muda nao.
vilevile, kama kuna matusi yameandikwa either kwenye msg za simu, au kuna ushahidi wa kutosha wa kuvurumishiwa matusi na mnao mashahidi, mnaweza kwenda kurepoti polisi ili afunguliwe kesi ya jinai. lakini mkishaanza hayo yote, jueni kuwa mpo vitani, mnapambana na watu, ama zao ama zenu. mnaweza kushangaa mnavyozidi kupambana nao ndivyo mnavyozidi kumtangaza mama yenu na kusambaza uzushi huo zaidi, kukawa hasara zaidi kuliko faida...na mama yetu hadi aje asafishe jina miaka kibao itapita.
kuna jamaa yangu mmoja alishawahi kuzushiwa jambo kama hilo, alivyozidi kupambana na wale watu, ndivo habari zilivyozidi kusambaa zaidi, kama angelinyamaza zisingesambaa. au, aende kwa wazee aombe msamaha kama alifanya. kama hakufanya, pia aende kwa wazee wawakalishe ili wamwambia huyo mama asiendelee kusambaza uzushi. poleni sana, ila nakushauri usimtetee sana mama yako, kwasababu yeye ni mtu mzima, na asingeaga anapoenda kufanya jambo zuru au baya....samahani kama nitakuwa nimekukwaza.
View attachment 102822
View attachment 102822View attachment 102822
View attachment 102821View attachment 102821View attachment 102821