Naomba msaada gari yangu aina ya Toyota Porte Engine ku heat na kuzima ikiwa kwenye mwendo

Naomba msaada gari yangu aina ya Toyota Porte Engine ku heat na kuzima ikiwa kwenye mwendo

Habar wajuzi wa mambo tatizo hilo linahusiana na nini ?

Msaada please kwa mtaalam
duh gari linaover heat likiwa kwenye mwendo ni ajabu......
anyway sababu zinaweza kuwa nyingi
1.cheki je feni linafunguka.

2.coolant IPO ya kutosha.

3.je radiator aina leakage.

4.mafuta ya gearbox(atf) yapo ya kutosha maana yakiwa kwa kiwango kidogo hupelekea transmission kuheat na vilevile engine.

5.thermostat je inafungua na kufunga mara nyingi inaweza kuwa imestuck kwenye close position.

6.Kama gari la zamani sana au limetumika kwa muda mrefu pasipo kufanyiwa service kwa usahihi inaweza kuwa radiator njia zake baadhi zikawa zimeziba so kasafishe radiator hii hutokea kwa gari zinazowekwa maji kwenye radiator
 
Habar wajuzi wa mambo tatizo hilo linahusiana na nini ?

Msaada please kwa mtaalam
Utaikaanga hio engine master. Awali ya yote kwenye mfumo wa upoozaji kuna shida. Angalia mfuniko wa radiator, feni kama inawaka na kuzima, level ya coolant ama maji. Au radiator enyewe inaeza kua na shida
 
Habar wajuzi wa mambo tatizo hilo linahusiana na nini ?

Msaada please kwa mtaalam

Asilimia kubwa ya magari Ikioverheat mwisho wa siku lazima itazima.

Cha kupambania hapo ni kwanini gari ina overheat?
 
Tatizo gari ina over heat, sensors zinapeleka info kwenye computer na kwa usalama wa engine wame design kukata moto. Je inawaka baada ya kupoa?

Nimeshawahi kuelezea humu ndani mechanism ya baada ya kuoverheat kwanini gari izime? Hapa nazungumzia asilimia kubwa ya magari including hilo la mtoa maada.

Actually kinachofanya gari izime ni engine kutengeneza space baina ya Cylinder head na block [EXPANSION], kwa sababu ya joto block na head zinapinda na kuachia nafasi. Gari itamisi itazima.

Na ikizima ukiiwasha haitawaka.

Ikishapoa [Contraction] ndio itaweza kuwaka.

Ndio maana gari ikioverheat mara kadhaa, tatizo la kuoverheat linakuwa la kudumu. Kwa maana space baina ya Block na head haitojirudi kama ilivyokuwa mwanzo.

Hivyo gari itakuwa inamiss, Air bubble kwenye radiator cap n.k.

Mwenye uelewa wa elasticity hii knowledge anaielewa vizuri kabisa.
 
Habar wajuzi wa mambo tatizo hilo linahusiana na nini ?

Msaada please kwa mtaalam

Utujie na majibu ya maswali yafuatayo?

1. Je maji yanapungua?

2. Radiator fan inawaka na kuzima?

Ukijibu hayo maswali mawili tunaweza kujua kwa kuanzia. Inaweza ishu ndogo tu.
 
Tatizo gari ina over heat, sensors zinapeleka info kwenye computer na kwa usalama wa engine wame design kukata moto. Je inawaka baada ya kupoa?

Yes inawaka na inatembea umbali mrefu kabla ya ku heat tena
 
Yes inawaka na inatembea umbali mrefu kabla ya ku heat tena
Yako mambo kadhaa ya kufuatilia.
1. Coolant/Maji yanapungua?
(a). Yanamwagika chini - hii utajua mahali unapopaki gari muda mrefu mfano nyumbani asubuhi. Dalili ya unafuu.
(b). Yanapungua bila kumwagika. Dalili mbaya.
2. Coolant haipungui ila inapata moto na yanachemka na geji inaonyesha kupanda sana.
(a). Inawezekana kuna shida ktk mfumo ama pump, thermostat au radiator
3. Coolant haipungui, joto la kawaida ila geji inapanda
(a). Mfumo wa upozaji wa kielektroniki, yaani sensors zimeharibika zinatoa taarifa za uongo kwenye computer.
 
maji yakipungua maana yake kuna mahali yanavuja.
Ni kweli, ila kuna kuvujia kwa nje, ambayo unayaona yame/namwagika au kuvujia ndani, hii ni ama yaingie kwenye oil au yaungue na mafuta. Mbaya zaidi ni kuchanganyika katika oil. Hizo mbili unaweza kulitumia gari kwa uangalizi wa ziada ila hiyo ya kuchanganya ni lazima silinda hedi ifunguliwe haraka.
 
Yes maji yanaweza kuvujia nje au ndani ya engine.

Ndani ya engine maji yanaweza kuvujua kupitia cylinder head gasket au Oil cooler.

Yakivuja kupitia Cylinder head gasket. Tegemea moshi mweupe, Gari kukosa nguvu[Au misi isiyoisha, Japo siyo mara zote], Bubbles kwenye mfuniko wa rejeta na mara chache sana Oil kuchanganyika na maji(Nasema mara chache kwa sababu kwenye engine nyingi njia ambayo Oil inapita kwa presha kutoka kwenye block kuja kwenye cylinder head iko moja tu. Njia nyingi huwa ni za Oil kushuka na haishuki kwa presha).

Maji yakivuja kupitia Oil Cooler, straight forward utayakuta mafuta kwenye rejeta au maji kwenye Oil. Hiki kitu watu huwa wanakipuuza na mwisho wa siku wanajikuta wamefungua cylinder head gasket kwa masaa wakati ni ishu ya Oil cooler.
 
Somo zuri. Tuanzie hapo maji kua na bubbles kwenye radiator tatizo hasa linakua ni nini?
 
Kwani coolant inatakiwa ibadilishwe baada ya muda gan??
 
Back
Top Bottom