Naomba msaada juu ya uso wangu

teenwolf

Senior Member
Joined
Feb 12, 2017
Posts
122
Reaction score
76
Uso wangu ni wa mafuta na hua nakua na chunusi. Tangu nipo na miaka na 13 hadi leo am 23,hua zina jaa na kupungua,pia break outs za hapa na pale ila dark spots haziachagi. Recently zimejaa sana kuliko kawaida na zinaanza kuacha dark spots.

Hospitali moja walisema ni allergy nyingine hormonal imbalance.
Nimetumia dawa lakini bado sema zmepungua tu kidogo.

Naenda miezi miwili sasa uso wangu hauna matumaini. Sina amani kazini nakosa raha hata kukutana na watu.

Nimesikia KCMC wapo vizuri,kama kuna mtu anayeweza kunipa mawasiliano ya huko naomba please.
Am ready hata kufanya surgery,nimechoka.
 
Same problem here, ila mimi zinaanza kutengeneza cysts na lipomas. Tayari nimefanya surgery moja. Ila nimekuja kugundua ukisugua kabisa na dodoki na kulala uso mkavu kabisa huwa inazipunguza kiasi
 
Same problem here, ila mimi zinaanza kutengeneza cysts na lipomas. Tayari nimefanya surgery moja. Ila nimekuja kugundua ukisugua kabisa na dodoki na kulala uso mkavu kabisa huwa inazipunguza kiasi
Surgery imekusaidia???
 
Jaribu natural home made therapy. Mtafte arabian queen kuna thread ameanzisha ya kutumia vitu vya natural kwa ajili ya ngozi.
 
Mazaga yote hayo nshatumiaga
Hadi hayo ya arabian queen?

Basi mm nikuongezee ya mwisho.
Asali vijiko 2 vya chai
Green tea kijiko 1 cha chai
white vinegar/ apple cider vinegar/limao/ndimu kijiko 1 cha chai.

Changanya huo mchanganyiko upake usoni au sehem iliyoathirika na vipele ukae nayo kwa mda unaotaka haina madhara hta ukiamua kulala nayo.

Baada ya wiki kama unapaka kila siku utaona tofauti. Chunusi zinaisha na sura inapata mngao
 
Hayo yote tayari plus ma cream yote
 
Ninaomba nione picha nijue how to help
 
Piga picha upande mmoja usioneshe macho pua wala mdomo tuone! Ili tujue umeathirika kiasi gani

Ushauri wangu : Jikubali jiamnini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…