Napia Kuku Wakiwa na Mafua Kitunguu Swaumu Unatumia kama Nilivyokuelekeza Hapo juu
Kitunguu Swaumu hutibu Zaidi ya Magonjwa 18+ Ya Kuku na Pia huwa Ni Kinga nzuri sana kwa kuku kwa wakati wote.
kumsaidia kuku anayeumwa mafua
Kuku akiumwa mafua yaani hapa anakuwa kama mzungu huu ni ugonjwa mbaya sana kwakuku hata ukimuona unamuonea huruma kabisa na hu ni ugonjwa unaoua kimya kimya kuku mara nyingi unaamka asubuhi unakuta kuku kakauka tayari na Mara nyingi huwa unaambukiza kwa kasi kidogo usipowawahishia tiba.
na Ukiwa umemwanzishia dozi ya kitunguu swaumu basi kuku hawezi kueneza hayo mafua kwa wengine(Na Hao Wengine Ukiwa umewawekea utaratibu wa kunywa kitunguu swaumu katika maji yao)
1.Chukua stiki ile ya kujichokonolea kwenye meno ukila nyama ikanasia ama kitu chochote japo wengine huweka kama pambo tu Unamshika kuku unamwangaliza kwa mbele ukiwa umekaa katika kigoda au stull(kimo hicho ndio utamsaidia kuku vizuri) Mkia wake unakuwa tumboni kwako na kichwa mbele basi unamshika kichwa unakuwa unamsaidia kuzibua pua maana mara nyingi huwa zinaziba.
Unazibua kwa kubonyeza juu ya pua ya kuku kama unapangusa hivi ukitumia pembeni sio kwenye ncha(Mfano kama mama anavyosukuma chapati vile ndio unatumia pembeni humo mwa stiki kubonyeza pua a kuku na utaona mafua uchaufu ukitoka ambao ulikuwa umeziba) Huku akimnywesha kitunguu swaumu
2.mara zote kuku pua zikiziba utamtambua atakuwa ni mpole sana na anakuwa anatabia kama ya kupiga chafya mara kwa mara huku akizungusha kichwa chake, Mda mwingine huchokonoa kwa kutumia makucha yake japo huwa hafanikiwi mara zote, huwa hali sababu anakosa uwezo wa kupumua vizuri ukimshitua mara moja unamuona anachanamka kidogo lakini ndani ya dakika hiyo hiyo anaduwaa tena haendelei kula.
basi Utajua tuu huyu shida ni hiyo na utamsaidia kama hapo mwanzo.
Kuku kufuga ni raha sana yaani asikuambie mtu ila wakiwa na usimamizi mzuri
Nimefuga sana kuku ila madawa ya kisasa mengi huwa yanguvu katika kinga kuliko tiba
na tiba nzuri ipo kienyeji kuliko kisasa
Namimi NIlifuga sana Kuku wa Kienyeji Kuliko Wa Kisasa Maana Wakienyeji Walikuwa na Faida Kubwa Kwangu
napia Kuku wa Kienyeji Sio Ndio Anastahimili Sana magonjwa bali Ukipata Kuku Chotara Jogoo wakisasa+Teta Wakienyeji=Product yake Ndio Hustahimili Zaidi magonjwa