Naomba msaada mahali ninakoweza kuipata hii dawa DINOPROSTONE 3MG. ni muhimu mno!

Pendaelli

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
11,050
Reaction score
31,412
Wakuu nawasalimuni sana, naomba msaada kwa hili ndugu.

Nimeshazunguka hii dar mpaka nimechoka kila duka halina hii dawa.

Ni ya kumsaidia mama mjamzito kujifungua kwa maelekezo ya daktari ameshaitiliza siku za kujifungua kwa hio hio dawa itakuwa ni ngumu sana kujifungua. naombeni sana wa kuu.
 
Utaua bure,mpeleke hospitali mgonjwa wako kuna dawa zingine haziuzwi madukani
 
Mkuu nenda agakhan hospital dar es salaam
 
Pole sana mkuu afu inaitwa dinoprostone it's vaginal tablet used to induce labour
 
nashukuru mkuu nitaipata wapi ndugu
 
Kwani hakuna dawa nyingine za kuinduce labor tofauti na dinoprostone?Mbona oxytocin ziko nyingi tu ila zinatoka kwa prescription

Mwambie huyo daktari awasiliane na mfamasia wa hiyo hospital apewe ushauri wa dawa mbadala za kuamsha uchungu.
 
mpaka sasa yupo sinza siku ya 3 mkuu nani dactar ameshauri hivyo
Sinza kwenye maelfu ya baa?

Anyway sisemi sana ila jipange next time upate hospitali nzuri na daktari,

Komaa nao labda wanataka hela ya supu,wapeeeee,usifate ya wana siasa,nchi yetu kusaidiana,wape hela ya OMO kufulia makoti,maafande tunawapaga ya kiwi,
 
Kwani hakuna dawa nyingine za kuinduce labor tofauti na dinoprostone?Mbona oxytocin ziko nyingi tu ila zinatoka kwa prescription

Mwambie huyo daktari awasiliane na mfamasia wa hiyo hospital apewe ushauri wa dawa mbadala za kuamsha uchungu.
nashukuru sana ndugu yangu hakika hii walio tuandikia nimeanzi kariakoo sinza manzese mwenge tegeta mapaka bunju kwa kweli wamesema hio dawa hawanayo.
nitakwenda kuomba ushauri kwa huyo daktari kama anaweza kubadilisha. asante sana mkuu
 
Usiwe mgumu tenga tu wekundu wa 5 mpe afanye mambo usiwafuate wanasiasa
 
laiti ndugu yangu ningepata hio nafasi ya kumpa chochote huyo mhudumu au dactari nisingejiuliza mara 2 lakini sina uzowefu sana na hii dar ndio maana nahangaka mkuu.
 
Kanunue mbadala yake inaitwa Photosynthesis......πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
mpaka sasa yupo sinza siku ya 3 mkuu nani dactar ameshauri hivyo
Siku 3 mmemuweka mgonjwa hospitali?

Ikishindikana kawaida kamfanyieni operation...kama hawana iwezo pelekeni hospitali inayowezekana

Mtakuja poteza mama na mtoto bure....kuzaa kawaida sio ushujaa


Ila kama yupo hospitali ya serikali zungumza vizuri na manesi na madaktari.....uhai wa mama na mtoto muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…