Kuna automatic ambapo Mayai hujiegeuza yenyewe na manual ambapo utakuwa unageuza Mayai Wewe kwa muda maalumu, zipo zinazotengenezwa ndani ya nchi japo sijajua kama hawa watengenezaji wa ndani wanaweza tengeneza zile automatic, na pia zipo kutoka nje ya nchi kuna mawakala wa makampuni, bei hutofautiana hazipo sawa kwa wote, ubora pia hutofautiana.
Sijawahi zitumia za ndani ya nchi Mimi natumia automatic na manual lakini zote ni imported.
Nitakupa mawasiliano ya watengenezaji na wauzaji wa ndani na nje ya nchi kwa PM mtajadiliana utaamua mwenyewe kulingana na mahitaji yako....
Haya makampuni ya nje yenye mawakala hapa nchini mostly wanagharamia wao wenyewe usafirishaji na mengineyo mpaka mzigo ukufikie.