Lengo lako ni nini? Usitake ushauri kwa mtu asiyejua lengo lako.Si busara pia kupokea ushauri kwa mtu usiyejua hata msimamo na malengo yake yeye binafsi.Ukishauriwa na walioshindwa utaishia kushindwa.
Wewe unajua kiasi cha fedha unazohitaji kufikia unachokitaka.Jihoji ,je ukiwauza utasogea kwenye lengo? ukiwaacha waendelee kuzaliana je una mabanda ya kutosha kuwatunza watakaozaliwa,utamudu kuwapa chakula ili usipoteze ubora wao.
Kuhusu soko ni jukumu lako kutafuta na kulijua kabla ya kuzalisha chochote.Hongera kwa kuthubutu kama unamaanisha na huigizi kuwa umechukua hatua uliyoifikia.