mkulima101
Member
- May 23, 2017
- 10
- 5
Fanyeni fasta!Habari za Majukumu,
Naomba kufahamishwa namna/hatua za kufuatwa ili kuukana Uraia wa Mtoto Mtanzania aliyepo Tanzania. Mzazi wake Mmoja ni Mtanzania na mwingine sio Mtanzania.
Natanguliza Shukrani.
Nyongeza:
Mtoto amepewa Uraia wa Mzazi Mwingine ambaye Sio Mtanzania.
akichukua uraia wa hiyo nchi nyingine automatically atakuwa ameukana uTanzania
Hapo naona mshachoshwa na huyu baba, sasa mnataka muondoke tu hapa nchini kihalal kabisaaaaa
Mtoto yupo Tanzania ila unataka uukane uraia wake ili aishi Tanzania kama mgeni?
Mtoto chini ya miaka 18 anaweza kuwa na uraia-pacha, kadhalika kutumia pasi ya TZ au ya nchi nyingine kwenye safari zake. Akifika miaka 18 na Kama ataamua kuwa raia wa nchi nyingine automatically atakua kajivua uraia wa TZ, huhitaji kufanya kitu chochote labda kuichoma pasi yake au kuitunza kama kumbukumbu au kuirudisha uhamiaji Kama uta wiwa na muda ukikuruhusu.