Naomba msaada nataka kuagiza gari

Naomba msaada nataka kuagiza gari

MKIBAIGWAsharkss

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2017
Posts
572
Reaction score
1,331
Wakuuu nimejichangachanga nataka kuagiza Toyota Raumu naomba wataalam msaada wa mambo mawili

1. Naomba waliowahi kununua gari kupitia Hizi website mbili

Realmotor.jp na
Sbimotor.com
Nimeangalia humo nimekuta Wanauza magari cheap sana ila sijasikia watanzania wakizitaja hizi website. Naomba wazoefu wanisaidie

2. Naomba kujua kama ni muhimu sana kulipia insurance na inspection nafikiria kuvitoa vyote viwili au kimoja ili kupunguza garama.

Ahsanteni sana
 
Mkuu site bora na namba moja ya kuagiza magari ni (BEFORWARD) kuhusu insurance huwezi kukwepa lakini pia kwenye site watakuonesha gharama zote mpaka gari inakufikia mkononi hamna janja za clearance kwa Agent bandarini wala nini....We ingia beforward.jp website unapoweka ODA yako weka BFS ID namba hii (2392410 ) unapata discount nzuri tu kwa msaada zaidi DM
 
Wewe mod uliefuta comment yangu unaona nafaidi m**** wewe[emoji35][emoji35]

Futa tena basi nipige ban uridhike


Mkuu site bora na namba moja ya kuagiza magari ni (BEFORWARD) kuhusu insurance huwezi kukwepa lakini pia kwenye site watakuonesha gharama zote mpaka gari inakufikia mkononi amna janja za clearance kwa Agent bandarini wala nini....We ingia beforward.jp website unapoweka ODA yako weka BFS ID namba hii ( 2392410 ) unapata discount nzuri tu kwa msaada zaidi DM

Mod acha roho mbaya

Mwl nashukulu kwa maelezo ila option ya kuagiza bila insurence
 
Bima lazima ulipie mkuu, lakini inspection siku hizi hazilipiwi sababu gari huwa inakuja kukaguliwa huku Tanzania na tbs ambayo utalipia 350,000. hizo site ulizotaja zote ni nzuri na zina magari mazuri, wewe chagua gari unayopenda mwenyewe maana mtumiaji ni wewe, acha kusikiliza watu wanaovutia biashara za site zao mkuu.

Kwa chochote na msaada wa ushuru unaweza ni DM pia nitakushahuri na kukusaidia wala sihitaji hela yako
 
Chukua tahadhari mkuu website zingine matapeli, ukishalipa wanapotea. Mimi nishalizwa na sikuweza pata msaada hata kwa ubalozi wa Japan hapa nchini hawakuwa na la kufanya. Chukua tahadhari sana na website gani una deal nao.
 
Chukua tahadhari mkuu website zingine matapeli, ukishalipa wanapotea. Mi nishalizwa na sikuweza pata msaada hata kwa ubalozi wa Japan hapa nchini hawa kuwa na la kufanya. Chukua tahadhari sana na website gani una deal nao.

Nashukuru kwa maelezo kaka.

Mimi nimeipenda hii website realmotor.jp ina magari mazuri cheap sana nimeona hata kuna kampuni ya Tanzania (tele motors) wananunua kwao
 
bima lazima ulipie mkuu, lakini inspection siku hizi hazilipiwi sababu gari huwa inakuja kukaguliwa huku tz na tbs ambayo utalipia 350,000. hizo site ulizotaja zote ni nzuri na zina magari mazuri, wewe chagua gari unayopenda mwenyewe maana mtumiaji ni wewe, acha kusikiliza watu wanaovutia biashara za site zao mkuu.

kwa chochote na msaada wa ushuru unaweza ni DM pia nitakushahuri na kukusaidia wala sihitaji hela yako

Nashukuru kwa ushauri nitalipia bima tu. Nashukuru pia kwa kunihakikishia kuwa website hizi hazina shida (realmotor.jp)
 
Mwl nashukulu kwa maelezo ila option ya kuagiza bila insurence
Unachokitafuta utakipata?
Unajua docs za kuagiza gari?
Kwanza unaitoa wapi?
Ulaya?
Singapore?
Japan?
Kama hujawahi kabisa tumia agency zenye ofisi hapa bongo.

Ila kama huna cha kupoteza go ahead.

Utakapotumiwa shipping line na makorokoro yake ukute JAAI imefojiwa au kuisha muda wake ndio utajua hujui
 
Nashukuru kwa maelezo kaka.


Mimi nimeipenda hii website realmotor.jp ina magari mazuri cheap sana nimeona hata kuna kampuni ya tz (tele motors) wananunua kwao
Kwanini usiwatembelee hao wakupe maelekezo?
 
Njoo kwa mwamba msuya na shimbo motors, wapo fresh sana, hutojuta
 
Unachokitafuta utakipata?
Unajua docs za kuagiza gari?
Kwanza unaitoa wapi?
Ulaya?
Singapore?
Japan?
Kama hujawahi kabisa tumia agency zenye ofisi hapa bongo.

Ila kama huna cha kupoteza go ahead.

Utakapotumiwa shipping line na makorokoro yake ukute JAAI imefojiwa au kuisha muda wake ndio utajua hujui

Kiongozi nashukuru kwa ushauri, gari naagiza Japan.

Kingine unatakiwa ujue sio mweupe kivile kuagiza vitu kutoka nje.nilitaka tu kupata more experience kwa wadau.
 
Kiongozi nashukuru kwa ushauri.gari naagiza japan .

Kingine unatakiwa ujue sio mweupe kivile kuagiza vitu kutoka nje.nilitaka tu kupata more experience kwa wadau.
Kila la heri Mkuu hayo yalikuwa mawazo yangu tu
 
Habari wadau,

Napita tu wadau, nasambaza upendo huu kwa wafanya biashara/makampuni tusiingie hasara;

31March ni deadline (siku ya mwisho) kufanya MAKADIRIO YA KODI. siku moja ya kuchelewa faini 225,000/=
KWA MSAADA ZAIDI NICHEKI 0788104228

ALARM.JPG
 
Back
Top Bottom