Naomba msaada nauli ya Namibia

lukala

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
594
Reaction score
590
Habari wanabodi naomba msaada ,mwenye kujua gharama ya usafiri kuelekea Namibia anielekeze
 
Kwa ndege au kwa bus? Kama ni kwa bus, unapanda bus mpaka tunduma tsh 40000 then itabidi ulale maaana utafika tdm saa nne usiku, usiku huo huo gonga passport cause border ni 24hrs, halafu asbh unapanda bus la ki zambia kwenda lusaka nauli yake ni roughly tsh 50000 which means usiku ule utaofika tdm u change kwacha, lusaka utafika saa sita usiku kama ni msafir usichukue lodge lusaka utalala hapo hapo stand yao ya bus inter city its much better than our ubungo, then kesho yake alfajir unapanda bus kwenda sesheke hiyo iko border ya zambia na namibia ni mwendo wa siku nzima naul mpaka kule border ni roughly tsh 40000 you will pass by livingstone then you go sesheke, hapo utalala asbh unakula vi tax ni kama buku mbili mpaka border, sasa sijui unaenda namibia which side???
 
Japo mimi sio mtoa mada ila nina safari kama hiyo mwezi ujao, naomba muendelezo kwa uwa umesimama kuelezea kwa kutokujua mtoa mada anaelekea upande upi wa namibia,
Safari yangu ni ya walvis bay! !
Nasubiri
 
Thanks japo sio mtoa mada ila umenisaidia pia,
Kwa ushauri wako.ni bora nikasafiri hadi livingstone ndo.nitafute connection za windhoek?
 
Ok asante sana mkuu, Naona ni kama wastani wa siku tatu kwenda huko kutoka Tunduma,
Umeshawahi kujua changamoto za kuendesha kutoka Namibia kuja Tanzania pia?b,nasikia kuna jangwa ni kweli?
 
Asante sana , ngoja nimtafute huyo stralis anipe mawili matatu,
 
Gabarone fika mpaka lusaka ,utapanda basi mpaka livingstone , hapo utapata mabasi mengi tu yanayo kwenda huko kupitia francis town, ni mwendo wa kutwa nzima kutoka livingstone
 
Japo mimi sio mtoa mada ila nina safari kama hiyo mwezi ujao, naomba muendelezo kwa uwa umesimama kuelezea kwa kutokujua mtoa mada anaelekea upande upi wa namibia,
Safari yangu ni ya walvis bay! !
Nasubiri
Naelekea kavanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…