Naomba msaada nijue namna ya kudai haki yangu kwenye hili

Naomba msaada nijue namna ya kudai haki yangu kwenye hili

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Wakuu naomba nisaidiwe.

Nimetoka Mwanza Leo August 5 na basi la Kampuni ya Kapriconi lenye namba za usajili T 320 ADC tukiwa tunaelekea Mbeya.
Tumefika saa 3 na nusu usiku , ghafla gari ikaamua kuishia iringa na Sisi abiria kuambiwa tupande coaster na ikaondoka fasts.

Kwenye Kosta mlangoni wanadai tiketi za kwenye Kapriconi na Mimi Kwa sababu ya kushuka ghafla tiketi nilisahau kwenye Siri.

Kwa hiyo nimetakiwa kulipa tena nauli ya Iringa -Mbeya.

Naomba kujua naanzia wapi kudai haki yangu maana pia nimeshalilika na kufedheheka.
 
Wakuu naomba nisaidiwe.

Nimetoka Mwanza Leo August 5 na basi la Kampuni ya Kapriconi lenye namba za usajili T 320 ADC tukiwa tunaelekea Mbeya.
Tumefika saa 3 na nusu usiku , ghafla gari ikaamua kuishia iringa na Sisi abiria kuambiwa tupande coaster na ikaondoka fasts. Kwenye Kosta mlangoni wanadai tiketi za kwenye Kapriconi na Mimi Kwa sababu ya kushuka ghafla tiketi nilisahau kwenye Siri.

Kwa hiyo nimetakiwa kulipa tena nauli ya Iringa -Mbeya .

Naomba kujua naanzia wapi kudai haki yangu maana pia nimeshalilika na kufedheheka.
Haki yako ilikuwa kwenye ticket kiongozi
 
Supporting document matters,, hapo huna namna mkuu… lipa tu & pole sana
 
Huna namba za agent ili athibitishe kule kwenye kitabu cha risiti?

Halafu kwanini wanafaulisha kizembe ivo ...usitoe pesa baki hapo mpaka mwende kituo cha polisi ...

Maana kama Huna pesa zingine utawapa nini ... kwanza ni kosa kumdhalilisha mtu
 
Kama tangu mwanzo wa safari ulilipia safari ya mbeya na gari exactly ni ya mbeya bt ikakatisha route basi una haki zote za msingi za kudemand your right ya kufikishwa destination uliyolipia .
 
INA MAANA MMEFAULISHWA?

JE SABABU YA NYIE KUFAULISHWA NI NINI!

ova
 
Wakihitaji supporting document wambie wampigie mtu wa kapricon angalie document zako kwwnye kitabu cha risiti watajie na jina ulilo andika
 
Huna namba za agent ili athibitishe kule kwenye kitabu cha risiti? Alafu kwanini wanafaulisha kizembe ivo ...usitoe pesa baki hapo mpaka mwende kituo cha polisi ... maana kama Huna pesa zingine utawapa nini ... kwanza ni kosa kumdhalilisha mtu
Point

Utafaulishwaje kizembe

Ova
 
Waeleweshe taratibu watakuelewa, usijifanye mjuaji, watakuzingua!
 
ndio tatizo la kupanda magari ya kampuni uchwara ambazo zina jifanyia biashara kiholela holela.

Halafu utakuta umetwangwa nauli kubwa kama ya mabasi ya VIP kumbe umepanda gari daraja la ordinary...
 
Hakuna sababu , wameamua tu na gari imeondoka haraka sijui imeelekea wapi
Hapo kuna harufu ya kuibiwa .. utapeli wa wazi wazi ... ingekuwa ni mimi kwanz kwenye hiyo kosta sishuki pia sitoi pesa wao wawasiliane wangalie kwenye kitabu cha risiti ... au twende kituo cha polisi tuka malizane ... what if huna budget ya kutoa pesa nyingine utawapa nini
 
Kuna chama cha kutetea Abiria ila hata sijui wanapatikana vipi, na hizi ndio ishu wanazopaswa kudili nazo...suala la kuwafaulisha ni makosa.
 
Kama konda wa bus naye amefaulishwa ongea naye atakukumbuka akutambulishe, unless pole sana
 
Huna namba za agent ili athibitishe kule kwenye kitabu cha risiti?

Halafu kwanini wanafaulisha kizembe ivo ...usitoe pesa baki hapo mpaka mwende kituo cha polisi ...

Maana kama Huna pesa zingine utawapa nini ... kwanza ni kosa kumdhalilisha mtu
nakazia hapa.
 
Binafsi basi namba A,B na C sipandi ng'o pesa nitafute kwa shida bado niitumie kwa shida,, never
 
Binafsi basi namba A,B na C sipandi ng'o pesa nitafute kwa shida bado niitumie kwa shida,, never
Mwanza - Mbeya ndio gari hizi hizi mkuu.

Nimenuia sitapanda tena gari ya moja Kwa moja Bali nitakuwa napanda Shabiby mpaka Dom siku inayofuata napanda gar zuri la Dom - Mwanza
 
Back
Top Bottom