Naomba msaada nini tiba kwa mama mjamzito kutema mate

Ndikwega

R I P
Joined
Feb 1, 2012
Posts
5,979
Reaction score
5,527
Habari wapendwa mm ni mama nina mtoto mmoja sasa nilipobeba mimba nilipata sana taabu sababu nilikuwa natema sana mate pia nimetema mate mpaka Siku ya kujifungua sasa naomba km kuna yeyote anayejua dawa ya hili tatizo
 
Chukuwa kikopo tia mchanga, uwe unatemea humo.unatingisha. kesho kingine tena
 
Ulikuwa unatumia supplements za vitamin? Pregnant care? Kuna watu wanatumia dawa kama Mega Prenatal na hawana yale mausumbufu ya mimba wanadunda tu
 
Ulikuwa unatumia supplements za vitamin? Pregnant care? Kuna watu wanatumia dawa kama Mega Prenatal na hawana yale mausumbufu ya mimba wanadunda tu

Hapana sijawahi kutumia aina yoyote ya dawa hivi kwani hayo madawa hayana madhara?
 
Ulikuwa unatumia supplements za vitamin? Pregnant care? Kuna watu wanatumia dawa kama Mega Prenatal na hawana yale mausumbufu ya mimba wanadunda tu

Zinapatikana hapa bongo? nijuze
 
Hapana sijawahi kutumia aina yoyote ya dawa hivi kwani hayo madawa hayana madhara?

Ni lazima kuzitumia kwani pia zinamsaidia mtoto kukua vizuri. Kiukweli inabidi Luanda mapema wakati unatafuta mimba lakini pia ni muhimu zaidi miezi mitatu ya mwanzo na unaendelea nazo kila siku na hata wakati wa kunyonyesha. Ni kidonge kimoja kwa siku kina vitu muhimu kama folic acid, Zinc, na madini na vitamins nyingine. Hazina madhara na ni lazima kutumia. Ukitumka hizi dawa hutakula udongo, wala kutema mate etc. Wengine hawatapiki toka mimba inaanza hadi wanajifungua. Mbona hata cliniki wanashauri inamaana hujawahi kuambiwa?
 
Zinapatikana hapa bongo? nijuze

Zipo brands tofauti tofauti na zinapatikana pharmacy. Ninayoifahamu sana kuwa ni nzuri inaitwa Mega Prenatal wanauza JD Pharmacy Mlimani City Tsh 15,000. Vidonge ni 30 dozi ni kimoja kwa siku au utakavyoelekezwa na daktari. Hivi vina hizo supplements 19. Unajua mimba inaleta mabadiliko mengi yakiwemo ya hormone sasa hizi vitamini au madini inasaidia kuweka sawa na kumsaidia mtoto kukua. Folic acid kwa mfano, inaepusha mtoto kuzaliwa na kichwa kilichojaa maji au mgongo wazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…