Naomba msaada, tatizo la kuanguka na kupoteza fahamu

kikii

Member
Joined
Jun 29, 2014
Posts
20
Reaction score
6
Habari zenu wanajamvi,

Mpaka naandika hapa kuhusu hili tatizo nililonalo la kuanguka na kupoteza fahamu ambalo lilinitokea kwa mara ya kwanza mwaka 2013 nikiwa na miaka 30.

Nilianguka ghafla tu nakupoteza fahamu kwa takribani dakika 10 na baadae fahamu zikarudi nikiwa nasikia mwili unauma na ukiwa umechoka sana.

Nimefanya kipimo cha MRI mara mbili pamoja na ECG mara mbili lakini hakuna dalili yoyote ya kifafa. nimekwenda kwa Prof Matuje lakini hakuna mafanikio na nimekuwa nikitumia dawa aina ya EPILIM kwa zaidi ya miezi sita.

Lakini hiyo hali imekuwa ikizidi kuniattack mara kwa mara bila kuwa na kipindi maalum, ilinisababishia hadi kupata ajali na kupelekea mtoto wangu akafariki na mke wangu kuvunjika taya la kulia.

Naombeni msaada kwa yeyote atakayesoma mada hii na kama anafahamu Doctor anayeweza tibu matatizo ya aina hii.

Asanteni
 
Pole sana mkuu.Jamani anaye elewa basi amsaidie mkuu huyu,piteni na hapa.
 
Mkuu pole sana.. hiyo inaweza ikawa inasababishwa na vitu vingi,vinavyopelekea damu kushindwa kufika seheme fulani ya ubongo.

Ingekuwa vyema ukachunguzwa hiyo mishipa inayopeleka damu huko kama iko sawa au vipi, fanya haraka, nenda muhimbili au bugando au kuna hospitali moja hivi ya wahindi iko mwanza,jina nimeisahau.

Kama inatokea mara kwa mara inaweza ikawa dalili ya stroke,chukua tahadhari,jitahidi kuacha matumizi wa dawa za maumivu (pain killers) labda ikilazimu sana..pia kipimo cha CT Scan kinaweza kusaidia kuona sehemu yenye tatizo hivyo ujieleze vizuri iki dokta aone umuhimu ya wewe kufanyiwa hicho kipimo.
 
Dawa yako ni Mungu. Lazima toka 2013 umezunguka kwa madaktari wengi, its about time to let God take the wheel, omba msaada kwake pia
 
Pole sana, angalia na uwezekano wa brain tumor, hawa wapimaji wa kibongo bana, watakuyeyusha tu, jaribu kwenda nairobi ukachukue vipimo
 
Seizure is a common symptom in people withbrain tumors. For some people, a seizure might be the first clue that something unusual is happening in thebrain. Seizures are particularly common with slow-growing gliomas, meningiomas located in the convexity of thebrain,and with metastaticbrain tumors.

02
A seizure is an attack caused by abnormal electrical activity in thebrain. It lasts only a short period of timeand maycause unusual movements, a change in the level or loss of consciousness,and/or sensory distortions. There are many different types of seizures. The type you experience depends on which area of thebrain has the abnormal electrical signals.
Below are some of the common features of seizures in patients withbrain tumors:
Sudden onset.

Loss of consciousnessand body tone, followed by twitchingand relaxing muscle contractions.
Loss of control of bodily functions.

At risk for biting tongue.
Short periods of no breathing (30 seconds); may turn dusky blue.
Short duration (2-3 minutes).
After effects include sleepiness, headache, confusion, sore muscles, brief weakness, or numbness.
 
Niliwahi kuwa na hili tatizo nikiwa na miaka 11 - 16 nikamuomba Yesu akaniponya sasa hivi niko imara kama Simba. Muulize Yesu. Afflictions come so we can know God the more, pray the more.
 
The two main reasons for blacking out are insufficient blood flow to the brainand abnormal electrical activity within the brain (a seizure).

While both of these sound scary, in reality most episodes of blacking out are not related to life threatening health problems.
This guide is designed to provide insight into why you passed out. It is not a diagnostic tool or a substitute for evaluation by a health professional.

The questions are ones your doctor is likely to ask you. Your answers provide a path to better understanding of the common reasons forlosing consciousness.
 
kikii

Unayo Pepo wa Kiuchawi ndio anaye kuangusha wewe ukiweza kunitafuta nitafute mimi ninaweza kukutibu na ukapona ukinitaka nikutibie bonyeza hapa.Mawasiliano
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…