Naomba msaada tatizo la kusinzia darasani

Joined
Jul 11, 2014
Posts
26
Reaction score
4
Habari wanaJF wote,

Nina umri wa miaka 19 npo kidato cha tano. Nipo hapa kuomba ushauri na msaada kuhusu tatizo langu la kusinzia darasani hasa mwalimu anapokua anafundisha, hasa mida ya mchana hivi ghafla usingizi mzito unanishika na hua siwez kujizuia mpaka mwalimu au rafiki yangu anishitue, hata hivyo tatizo la usingizi huendelea kunikumba........

Je ni tatizo la kiafya? Au ni nini chanzo chake japo usiku hua nalala muda wa kutosha tu... Msaada tafadhal mana hii hali nimeichoka na siihitaji iendelee kunitesa Mana mwisho wa kipindi usingizi huisha na hua naamulia patupu kwa kile mwl alichofundisha.
 

Attachments

  • young 4r_001.jpg
    23.5 KB · Views: 348
Usisumbuke sio tatizo kubwa sana na ukahofu kwamba litakufanya ufeli. Watu wenye kusinzia darasani wakipata muda ambao hawasinzii akili yao ina uwezo mkubwa sana ya kuelewa na kutunza kumbukumbu hivyo usiwe na hofu sana bado una nafasi nzuri sana ya kufaulu kuliko hata wasiosinzia darasani
 
pole sana kijana.. angalia na vyakula unavyokula kabla ya kuingia vipindi
 
What about Thyroid gland problems? People survive with it for some years without noticing
 


nilipokua chuo nilikua nabhili tatizo,bora yako mchana mi nikishakunywa chai tu ni usingizi mzito sana kwa kwenda mbele.mara nyingi vipindi vya kuanzia saa nne mpaka saa nane kwangu ilikua ni shida au siendi kabisa darasani .nadhani hili ni tatizo la kutokufanya mazoezi vizuri,kula vizuri na kunya maji mengi bila kusahau kulala kwa wakati.
 
Pole sana hii ni zaidi ya kawaida, nakumbuka hata mimi nilipokuwa high school nilikuwa nasumbuliwa sana na usingizi hasa mwalimu anapofundisha darasani.
Kijana unahitaji sana maombi ili kuondokana na tatizo hili. Hudhuria kanisa lolote la kilokole uombewe hii hali itaondoka na utakuja kuthibitisha hapa.
 

acha kumpotosha mwenzio
 
Jaribu kuwa na lengo madhubuti kwa kila kipindi kabla mwalimu hajaingia darasani.
Mfano, natamani kujua ............ na leo ndio mwalimu atafundisha, so ile ....... niliokuwa naishangaa leo lazima nikitoka niwe nimeipata vizuri, asipozungumzia nitamuuliza.
tayarisha maswali kama 3 ya kumuuliza mwalimu, au unaweza kuyapata anapoongea.

hapo ni baada ya kumuona daktari na kukujulisha huna ugonjwa kautisha.
Wengi husinzia pale wanaposhindwa kupata relevancy ya kinachozungumzwa na wao. au malengo yao. inawezekana bado hujajua hivyo vipindi vinauhusiano gani na malengo yako makubwa, nadhani unaviunganisha na lengo lakufaulu mtihani tu.
 
Kaa mbele yaani utizamane na mwalimu pia usaidie kufuta ubao jitahidi kuwa unauliza maswali hata kama ni pumba na pia kujibu maswali class we jibu tuu si unajua kuna ile dhana ya there is no right or wrong answer na wote mko kujifunza
 
Fanya mazoezi..pia tumia juice ya vitunguu thoumu nyakati za jioni...saga vitunguu thoumu vile vidogo sio vile vikubwa...una ulegevu wa mishipa sehemu ya ubongo wako kwa hio tumia vitunguu thoumu...unaweza hata kutafuna kama punje 3 ivi kila siku jioni kuanzia 10-12
 

Aiseeeeeeeeeee!!??
 
acha kumpotosha mwenzio
Hapana simpotoshi, kuna mambo mengine magumu kidogo kuyaelezea lakini ni ya kweli, kuna nguvu nyingi zinasumbua watu na hasa spirits kwa watu wa kiroho hii kitu wanafahamu sana.
 
Hapana simpotoshi, kuna mambo mengine magumu kidogo kuyaelezea lakini ni ya kweli, kuna nguvu nyingi zinasumbua watu na hasa spirits kwa watu wa kiroho hii kitu wanafahamu sana.

mbona hao ndio wanachochea hizo nguvu za giza.
 

mkuu wewe unaweza kunya hayo maji ?? au aharishe ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…