Naomba msaada wa Jinsi ya kukata kuku hatua kwa hatua

Naomba msaada wa Jinsi ya kukata kuku hatua kwa hatua

Claranito

Member
Joined
May 26, 2014
Posts
28
Reaction score
3
Habarini wana jamvi!

Binafsi napata tabu sana kumkata kuku vipande vipande, nikimkata nakata hovyo hovyo tu, naomba kuelekezwa jinsi ya kukata vizuri hatua kwa hatua.

Asanteni.
 
mimi kuna siku sitasahau,demu wangu aliniambia siku hiyo nimuandae kuku na kumpika,yaani ilikua ni vichekesho kwenye sufuria baada ya kumuivisha,ilikuwa hana shape aliopiva,vurugu kwenye sufuria,hizi kazi tuwaheshimu mademu zetu
 
hehhehe raha kula kumkata kuparangana..hahahh..mara mia kukata nachukia kumtoa manyoya,nikienda sokoni af hamna hyo huduma naweza ahirisha.nkanunua.nyama ingine tu
 
Hadi mkasi!!?????

yeah, tena huko mahotelini wanavokata hivi vikuku vya madawa ni mkasi tu. kuku wa kienyeji ni rahisi sana kufuata viungo tu kuongoa miguu na mabawa, baadae kunapasua tumbo kwa uangalifu unaenda shngoni unakamata koromeo unalishusha chini unavuta matumbo yote yanatoka mara moja, unaachanisha kidari unapasua katikati kazi imeisha. hakuna kitu rahisi kama kukata kuku, kazi ipo kwenye kunyonyoa, mimi nikinunua kuku nawaambia wanamtengeneza kabisa kurahsisha kazi, sema lazima usimamie, unaweza kuchagua kuku mkubwa ukawaambia wakutengezee utaenda kuchukua ukitoa mguu wako tu wanachinja kifaranga au wanakukatia kibudu kabisaa!
 
Ila sometimes unaona ni mkubwa kumbe manyoya tu mengi lol

hahaaa, ndiyo tatizo la kuku hilo, kakinyonyolewa unakakataa...lol! mimi huwa naangalia sana uzito, ukimnyanyuanyanyua unajua tu kama kana uzani, unakakagua tuhips kama tuna afya.
 
Baada ya kunyonyolewa muweke sehemu yenye nafasi tumia sinia au hata mezani, anza na kutoa kivuko cha chakula (uchafu pale shingoni, kivute vizuri kisitumbuke, akiwa chali toa paja na t.a.k. (yaani hips) mgeuze kifudifudi kama si mtaalam papasa katikati ya bega lake na mgogo kuna kifupa utakishika ingiza kisu sehemu hiyo pandisha juu kwenye maungio ya kipapatio kivunje toa pamoja na kipapatio halafu ingiza vidole gumba sehemu ulipotoa kipapatio (mshike mkono wako mmoja upande wa kifua mwingine upande wa mgongo) tenganisha tumbo na mgongo, vitu vyote vya ndani vitakuwa sehemu ya mgongo vitoe kwa pamoja kata vizuri nnya izidondokee kwenye nyama, tenganisha kiuno na kila wajinga (mbavu) hakikisha huyo kuku katoka vipande 9: paja 2, t.a.k.o (hips) 2, mgongo, mbavu (mgongo na mbavu hazikatwi mara mbili) vipapatio (mbawa)2, Steki ya tumbo 2. shingo peke yake 1. kama mlaji wa filigisi itumbue vizuri usitenganishe na maini hakikisha umetoa kifuko cha nyongo. hapo umemaliza kazi endelea na upishi wako.
 
Back
Top Bottom