Naomba msaada wa kisaikolojia

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Wakuu heshima kwenu.naomba nielezee tatizo langu.

Mimi ni kijana wa makaomo mwenye afya timamu sina stress kabisa lakini kuna jambo huwa watu wananiambia.ni hivi.

Nikiwa nimekaa na watu wengi katika maongezi watu huniambia siko pale kiakili,huniambia nina mawazo au nina stress nikiwaambia kwamba sina tatizo nipo kawaida,wananiambia mbona uko hivyo? Nakosa cha kuwajibu ila nahisi kwa sababu hizi ndo mana wanaona kama nina msongo..

1.Mimi sio muongeaji sana jambo ambalo linafanya mda mwingi nikiwa na warafiki nakuwa kimya sana japo wakati huo nakuwa kuna mambo ya kawaida sana nayawaza kimaisha,naweza kuwaza hesabu za maendeleo yangu naweza kuwaza wazazi n.k yani ubongo wangu unakuwa haujaconcetrate na stori za pale japo nikiulizwa naweza kuchangia mada pale lakini siwasikilizi ile kwa umakini

2.lakini pia hupenda kusngalia sehemu moja,yaani wakati nipo kimya kama naagalia sehemu naagalia sehemu hiyo hiyo mojaa sigeuzi geuzi shingo huku na kulee nakuwa nimetulia tu,nadhani ndo maana wanaona kama nina msongo wa mawazo.

sasa mimi naomba msaada wenu jee naweza kuwa na tatizo au msomgo kama wanavosema watu japokuwa mimi mwenyewe najiona nipo kawaida?


Lakini pia mimi sio mtu wa kufatilia baadhi ya mambo mfano naweza nikawa nipo mtaani alafu mtu nikawa namjua kwa sura tunaongea na yeye ananijua jina ils yeye nakuwa jina simjui,au naweza kwenda sehemu kama dar au zenj alafu kuna yale maeneo maarufu huwa hata sina mood ya kwenda huko mpaka watu wananiona tofauti jee hali hii inatokana na nini?
 
Mkuu upo write sana.

Ni vizur kuongozwa na kile ambacho unakihitaji, achana na hisia za kukupeleka hulu na huku,
Endelea ku focus to what you mind, ukikamilisha hicho kwanza katika maisha yako ni vizur.

"You have to train your mind to be stronger than your feelings or else you gone lose yourself"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu samahani naomba ufunguke zaidi.

Umeniacha kidogo katika hizo maneno za mwisho za kizungu naomba ufanye kunyumbua
 
Nakupa mfano;-
Mind ya mtu inaweza ikawa inamuongoza au inataka kufanya jambo fulaini zuri tu mfano unaweza kuwa ni mjasilia mali, mind yako inakwambia kuwa lazima uweke akiba ili kukuza mtaji wako.

Lakin hisia za mwili (feelings) mala nyingi ndio zinatupoteza binadamu, hisia zitakwambia unataliwa ukatafute wanawake kwa kuwapa pesa na wao wakuvulie chupi, au ukjikuta unapenda kunywa pombe kila siku, matokeo yake hata mtaji unaweza ukaupoteza wote.

Ukimuona Diamond au Harmonize anaenda Jimy, sio kwamba kapata hisia za kunyanyua vyuma, hapa anacho taka yeye awe na sex body, so itambidi aende tu kufanya mazoezi japo pia hisia zilikua zinataman muda huo aende kura raha na mzungu wake.

So, we focus na maisha yako vitu ambavyo ni positive na vina faida kwako sasa na badae,

Hisia za mwili sometime zinatupoteza tu.
safuher
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aiseee.mkuu unanifikirisha sana ujuee.


Ina maana niachane na wanayosema watu juu yangu nifanye mambo yangu tuu mkuu ama vipi?
 
Kuna game nataka nikufundishe ya kucheza it is a perfect game,safe game ambayo utakuongezea concentration yako na pia tunaweza kugundua Kama una stress au lah..Kama uko dar mitaa ya tabata, buguruni,ubungo nambie nikuelekeze wapi uje
 
Daah Siko dar mkuu.

Ila mbona napitiaga sana nyuzi mbali mbali naona kwamba dalili kubwa ya stress ambayo huwendo naona niko nayo ni kuqa napenda sana kuwa ndani peke angu.

Lakini naenjoy sio kwamba nakuwa ndani kiasi kwamba napata msongo wa mawazo ama naanza kuwaza mambo ambayo yataninyima raha,hapana.

Nakuwa ndani wakati ungine naweza kufungua feni au naweza kusoma kakitabu fulani,au naweza kuwaza juu ya maneno fulani katika kitabu fulani n.k

Lakini nikitoka nje naona washkaji wamekaa wanapiga soga na story za hapa na pale,sasa hapo huwa naingiwa na hofu kwa kujiuliza "mbona kama niko tofauti"?

Nikiumwa hapa atajua nani kama naumwa na huku kukaa peke angu?
Sasa nikijiuliza hivyo huwa mara moja moja natoka nakaa vijiweni,ila kiukweli kama ningekuwa na jambo linanisumbua ningejijua hapa mwenyewe.
Kuna game nataka nikufundishe ya kucheza it is a perfect game,safe game ambayo utakuongezea concentration yako na pia tunaweza kugundua Kama una stress au lah..Kama uko dar mitaa ya tabata, buguruni,ubungo nambie nikuelekeze wapi uje
 
Upo kama mimi yani tangu nikiwa mdogo nikiwa napiga story na watoto wenzangu huku tunatemvea kuna mda nasimama wao wanaenda mi nimesimama tu naangalia sehemu moja yani kama nasikiliza kwa makini vile
Walikua wananishangaa sana mpaka sasa nipogo ivo

sometimes... hasira zinanifanya nisibonge....
ikiwa rafiki wa karibu.. ndo anaefanya nisisonge ....
 
Dahhhh aiseeee
 
Una stress kubwa kuliko iliyowahi kumpata binadamu yeyote Afrika mashariki na kati
 
Unaumwa mdogo wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…