Zee la choji
Member
- May 15, 2016
- 56
- 122
Habari za muda huu?
Nilitafutiwa chumba na dalali maeneo ya Magomen Kagera pale maeneo ya Oil com, Hivyo basi nilitoa kodi ya miez 5 na Kodi ya 1 ya dalali jumla nikatoa tsh 360,000 kwasababu kodi ya chumba ilikuwa tsh 60,000.
Sasa baada ya wiki moja alikuja mtu wa makamo na kujitambulisha kuwa yeye ni mwenye nyumba, na hiyo nyumba ni ya kwake alinunua na ipo kwenye mgogoro ambapo kesi inaunguruma mahakamani hivyo basi hatakiwi mtu yeyote yule kuishi pale. Nyumba hiyo tulikuwa jumla ya wapangaji 2 tu.
Basi ikabidi tumfahamishe sisi tuko pale kihalali na kumuonyesha mikataba yetu ya kupanga, Lakin yeye alidai inabid tuhame tu. Tulichofanya tukampigia yule alietupangisha lakin hakuwa anatoa ushirikiano kwa kusema atatupigia baadae.
Kwahiyo tulichoamua mimi na mpangaji mwenzangu ni kumwita mwenyekiti wa serikali ya mtaa na balozi Ili atusaidie juu ya hilo sekeseke. Kwahiyo tutakaa kikao na hao viongozi tajwa hapo pamoja na mwenye nyumba.
Mwenye nyumba alikiri kumtambua huyo alietupangisha ambaye pia alikuwa anaishi hapo kama muangalizi wa nyumba lakin pia kwa mahusiano ni mtoto wa Babu yake.
Ndugu M/kitu akaamuru yule mwenye nyumba ampigie yule alietupangisha, M/nyumba alipompigia huyo muhusika alietupangisha. Huyo jamaa alipokea simu na alikiri kutupangisha sisi. Na huyo jamaa alietupangisha na muangalizi wa hiyo nyumba lakin pia huyo Mwenye nyumba ni mtoto wa Babu yake kwa uhusiano.
Basi makubaliano ya kikao yalikuwa turudishiwe fedha zetu Ili tuweze kuhama, Sasa Cha kushangaza leo nimerud kwenye shughuli zangu tumekuta mwenye nyumba amekata umeme pamoja na maji. Sasa ndugu zangu nipo njian ya panda nifanyaje.
Naomben ushauri