Naomba kujua kuwa sheria inanisaidia vipi kama mtumishi wa serikali, mimi ni mtumishi katika halmashauri mojawapo ila matatizo niliyo kutana nayo huku ni kuwa watumishi wengi wanalalamika kuhusu haki zao hasa watumishi wa chini nikiwepo na mimi, kwamba utakuta mtumishi anadai stahili zake kama posho ya safari,extra duty,meal allawance nakadhalika na taratibu zote anazotakiwa kufanya zimekamilika lakini matokeo yake utakuta hatulipwi kwa muda muwafaka inafikia kipindi hadi madai yanalundikana ya takriban miezi 4 hadi 5, bila ya kulipwa chochote ukiuliza unaambiwa OC bado haijaingia au halmashauri haina hela, jee kutokana na swala hili kisheria nitafanyaje ili niwe napata haki zangu kwa wakati....? Nihilo tu wadau naomba msaada wenu kwani sometime hadi najuta hata kuajiriwa serikalini