Nitasema kama mzazi! halafu na wewe fikiria kama mzazi! Hapa nafikiria scenerio moja tu ili kufupisha mazungumzo - nyingine zawezekana pia
Kweli ulawiti umetokea na mdogo wako kafanya hivyo! (Hii haimanishi kwamba mdogo wako hakuhusika na ulawiti huu - ya wezekana kabisa kundi lao zima wamesingiziwa na ulawiti huo ulitokea kwingine. Pili, yawezekana kabisa mdogo wako alishuhudia tu ulawiti huo ukitokea na mwisho yawezekana kabisa mdogo wako alikuwa kinara) Lakini kwa kuwa unatafuta wanasheria namba moja na mbili watayapembua kirahisi na kujenge utetezi ambao mdogo wako atakuwa huru. Ila iwapo namba tatu imetokea basi unakazi zaidi ya kulinda maslahi ya mdogo wako tu.
Cha kwanza kaa chini uongee na mdogo wako vizuri na kwa undani. Mtoe hofu na kumuahidi utamsaidia - (ingawa ingekuwa ni mimi mdogo wangu kafanya hivyo - kweli kabisa ningemuacha afungwe - afungwe afugwe- atapelekwa mahakama ya watoto kujifunza (ingawa pia katika jela zetu za sasa siamini kwamba sinamzaidia mfugwa kujifunza ubinadamu zaidi ya kumpa mateso). Ila wewe inaonekana unataka sheria imlinde mdogo wako hata kama anakosa - hiyo ni hiari yako na unahaki ya kuamua jinsi gani ungependa maslahi ya mdogo wako yalindwe. Sasa, ili mwanasheria aweze kumsaidia nilazima afunguke na itakuwa vyema kama atafunguka kwako. Nacho maanisha hapa, lazima ufungue nafsi yako na ukubali uhalisia na kosa iwapo mdogo wako katenda - si haki kutumia sheria tu kumaliza maswala ya ubinadamu.
Pili tafuta kuelewe kiini cha tabia hiyo katoa wapi - na basi kama anapaswa kuanza kubadilishwa afanyiwe hivyo. Maana mara nyingi, watoto wanaolawiti wenzao - mara kadhaa walishawahi kulawitiwa ama kushuhudia ulawiti wa aina hiyo - ama wanajihusisha na makundi ambayo yanafanya vitendo hivyo. Ama wengine ni misukumo ya miili yao - kwa hiyo ni vyema ungalie nje ya sheria tu. yawezekana kabisa unaweza kumlinda na sheria sasa lakini sheria ikamkamata baadaye. unaweza kumlinda na mtoto wa jirani baadaye akakamata wa ndugu! usijaribu kumaliza matatizo tu - fumbua na uwelewe tatizo ni nini? mtoto wa miaka 11 kupata wazo la kulawitii ni mapema sana - labda anaangali filamu za ngono! I will definetly be concerned with the sexual wellbeing of the young man!
Tatu, iwapo utajua ukweli, na kushauriana na mwanasheria wako - je unaweza kuwasialiana na mzazi wa mtoto aliyelawitiwa? Nadhani kunamichuko ya kibinadamu inapaswa kuangaliwa. Hata kama kesi inaendelea, na kama haitaingilia taratibu za kesi hiyo, kutoa pole kwa mzazi hata kwa mtoto pia ni jambo jema sana.
Hapa nataka ujiulize swali, iwapo mdogo wako angekuwa ni yeye kalawitiwa ungelifanyaje?