Naomba msaada wa kisheria kuhusu suala hili la makato ya mkopo

Naomba msaada wa kisheria kuhusu suala hili la makato ya mkopo

Kabla ya kuwashitaki waandikie barua ya kisheria(Demand letter) ya kuwajulisha kwamba kitendo walichofanya ni kinyume na sheria na makubaliano yenu wakati unafungua akaunti na ni kinyume makubaliano ya mkopo( loan agreement).

Katika barua hiyo waeleze ni kwa namna gani kitendo hicho kimekuathiri kiuchumi au kivyovyote na una nia ya kuwashitaki kufuatia kitendo hicho.

Kutokana na kuathirika huko waombe wakulipe fidia ambayo itakufanya ujihisi upo katika hali yako ya mwanzoni kabla ya kuchukua pesa zako kwenye akaunti yako bila ruhusa yako.

Wape siku 7 ili waweze kutia madai yako. Wasipofanya hivyo wafungulie kesi.

Kuhusu suala la kushinda ni kwamba ukiweze thibitisha madai yako basi utapata haki yako.

The most important thing is evidence. If you have some evidences to prove your claims and strongly establish your case you have overwhelmed chance to win.
 
naomba kujua yafuatayo;
1. niwaamdikie barua mimi mwenyewe au nitumie wakili?...
1. Tumia Wakili ili kuwaonesha kwamba upo serious sana na hivyo vitendo wanavyofanya. Hii itawashawishi waje make meza moja ili muone mnalimalizaje.

2. Hakikisha huo mkataba hauna kipengele kinachosema kwamba mkopo unawezwa lipwa na vyanzo vingine vya kipata.

3. Fidia unadai kiasi chochote mkuu. Hata Tshs 500,000,000/=

Unaweza tengeneza mazingira kama ifuatavvyo:-
a) Kama unafanya biashara waambie kwamba hiyo hela ilikuwa ni ya kulipia pango au kununua bidhaa hivyo imepelekea wewe kupoteza wateja wako au kufungiwa sehemu ya biashara hivyo umepata hasara.

b) Hiyo hela ilikuwa ya kulipia pango la sehemu ya biashara au pango la sehemu ya kukaa. Hivyo kukata hiyo hela kumesababisha migogoro.
 
Kabla ya kuwashitaki waandikie barua ya kisheria(Demand letter) ya kuwajulisha kwamba kitendo walichofanya ni kinyume na sheria na makubaliano yenu wakati unafungua akaunti na ni kinyume makubaliano ya mkopo( loan agreement)...
Nimeona kama wewe ni mtaalam wa mambo haya ya sheria na haki.

nina kisa kimenitokea leo tar 14 july 2021. Kesi iko hivi.

Nilinunua kiwanja Kimara mwaka 2018. Nilikaa nacho hadi 2019 nikaanza ujenzi. Jirani yangu kulikuwa na Kiwanja kidogo ambacho mmiliki akimuuzia mteja mwingine.

Kutokama kiwanja kilichouzwa kilikuwa kidogo mteja aliyenunua aliamua kujenga, mwanzo akawa anazidi mipaka yake na kuingia upande wangu. Nilimuonya akarejea nyuma kidogo. Sasa nina wiki kadhaa bila kutembelea sight leo nilipoenda nikakuta Amejenga kaingia mipaka yangu kama mita 2 hivi.

Yaani amevuka bikoni ambazo zinaonekana ziko wazi. Na hizi Bikoni nilipikiwa na baraza la ardhi la serikali ya mtaa na document ninazo na wao ndio waliozijenga.

Hebu nishauri nini cha kufanya? nimpige faini au nimpeleke mahakamani abomoe?

Natanguliza shukrani
 
Amani iwe nanyi!,

Wakuu nina mkopo katika bank fulani nchini na makato ya mkopo wao wanakata kwenye mshahara (maana mimi ni mtumishi wa umma).

Tatizo tokea mwezi wa nne wanakata pesa iliyopo kwenye account yangu,ila baada ya muda wanarudisha ( na nilitoa taarifa ndio ikarudi kwa maelezo kuwa systems yao imekosea)...
Naomba nkujibu mkuu, kwenye mkataba wako wa mkopo ulio saini una date ya kulipa marejesho sasa ile tarehe ya kulipa rejesho inapofika, system ina collect the amount available kwenye account kulipa rejesho.

Sasa kwakua wewe ni mfanyakazi wa umma ni kwamba makato yako yanakatwa moja kwa moja hazina then hazina wanatuma hiyo pesa ya maresho benk uliokopa kwa ajili ya system kulipisha hilo rejesho.. sasa kwa scenario uliovoelezea kwa thread yako kinacho onekana pesa haifiki kwa wakati kwenye system, matikeo yake system inachukua kilichopo kwenye account.

Lakini pesa ya makato toka hazina ikiingia muda fulan kabla ya muda system kuchukua rejesho maana yake ni kwamba ile pesa itakua tayar kwa system na muda wa ku collect ukifika system inachukua.

Sasa ukienda mahakaman kushitak unaweza ukafail kwakua wewe kwenye mkataba ulikwisha kubali kua utakua unalipa mkopo wako kila tarehe fulan, so kama hazina wanachelewesha pesa system haitaju hilo system yenyewe ipo programed kuchukua rejesho kutoka kwenye any available bank balance ya akaunti yako.kaeni chini wewe na benki na mwajiri wako m solve hiyo issue.
 
Back
Top Bottom